Ni shangwe za kutosha usiku huu ndani uwanja wa Nangwanda Sijaona mkoani Mtwara.
Msanii aliyeibuka kwa kasi hivi sasa katika muziki wa Bongofleva,aitwaye Snura akionesha staili ya Kuvurugwa jukwaani.
|
Add caption |
Baadhi ya Wakazi wa mkoa wa Mtwara na
vitongozji vyake wakiwa wamejitokeza kwa wingi kwenye tamasha la
Serengeti Fiesta 2013,ndani ya uwanja wa Nangwanda Sijaona.
Anaitwa Dj Mully B akionesha umahiri
wake wa kukamua mangoma mbele ya maelfu ya wakazi wa mji wa Mtwara
waliojitokeza kwa wingi kwenye tamasha la Serengeti Fiesta 2013.
Mashabiki wa tamasha la burudani la
Serengeti Fiesta 2013 wakifuatilia kwa makini yanayojiri kwenye tamasha
hilo usiku huu ndani ya uwanja wa Nangwanda Sijaona mkoani Mtwara,ambapo
wakazi wa mkoa huu kwa mara ya kwanza walishuhudia live tamasha hili
ambalo hufanyika mara moja kwa mwaka.
Wakishangweka safi kabisa.
Ni burudani ya kutosha kabisa usiku huu
ndani ya tamasha la serengeti fiesta ambapo maelfu ya watu wamejitokeza
kuburudika ndani ya uwanaj wa Nangwanda Sijaona mkoani Mtwara.
Anaitwa Linah kutoka nyumba ya vipaji ya
THT,akiimba jukwaani mbele ya umati wa wakazi wa Mtwara waliojitokeza
usiku huu kwenye tamasha la Serengeti Fiesta 2013.
Kijana mdomo,lakini anaonekana kuja kwa kasi kabisa katika anga ya
muziki wa kizazi kipya,hasa hip hop,aitwa kwa jina la kisanii Young
Killer kutoka jijini Mwanza,akitumbuiza usiku huu mkoani Mtwara kwenye
tamasha la Serengeti fiesta 2013.
No comments:
Post a Comment