RAIS JAKAYA MRISHO KIKWETE AKITEKELEZA MAJUKUMU YAKE KWA TAIFA.
RAIS Jakaya Kikwete amefanya mabadiliko ya uongozi katika ngazi za juu za
utendaji wa Serikalini kwenye nafasi za Makatibu Wakuu na Naibu Makatibu Wakuu
katika Wizara mbalimbali, ambapo wapo waliohamishwa, wataopangiwa
kazi nyingine na yumo anayestaafu.
Kauli hiyo ilitolewa leo jioni na Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Sefue
wakati akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam.
“Rais amefanya mbadiliko haya kwa lengo kuu la kuimarisha utendaji wa kazi za
Serikali katika ngazi hizo za juu,” alisema Balozi Sefue.
Mabadiliko yaliyofanywa kwa upande wa Makatibu Wakuu ni kama ifuatavyo:
- Dk Florens Turuka amekuwa Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu,
awali alikuwa Katibu Mkuu Wizara ya Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia.
- Joyce Mapunjo amekuwa Katibu Mkuu Wizara ya
Ushirikiano wa Afrika Mashariki, awali alikuwa Katibu Mkuu
Wizara ya Viwanda, Biashara na Masoko.
- Jumanne Sagini amekuwa
Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu - Tawala za Mikoa
na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) awali alikuwa Naibu
Katibu Ofisi wa Waziri Mkuu - TAMISEMI.
- Dk Servacius Likwalile amekuwa Katibu Mkuu Wizara ya
Fedha, awali alikuwa Naibu Katibu Wizara ya
Fedha.
- Dk Patrick Makungu amekuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya
Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, awali alikuwa Naibu Katibu
Mkuu katika Wizara hiyo.
- Alphayo Kitanda amekuwa Katibu Mkuu Wizara ya
Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, awali alikuwa Naibu Katibu Ofisi ya
Waziri Mkuu – TAMISEMI.
- Dk Shaaban Mwinjaka amekuwa Katibu Mkuu Wizara ya Uchukuzi,
awali alikuwa Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Viwanda, Biashara na
Masoko.
- Dk Uledi Mussa amekuwa Katibu Mkuu Wizara ya
Viwanda, Biashara na Masoko, awali alikuwa Wizara ya Ushirikiano wa Afrika
Mashariki.
- Profesa Sifuni Mchome amekuwa Katibu Mkuu wa Wizara
ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi, awali alikuwa Katibu Mtendaji
Mkuu wa Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania.
- Charles Pallangyo amekuwa Katibu Wizara ya Afya
na Ustawi wa Jamii, awali alikuwa Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri.
- Anna Maembe amekuwa Katibu Mkuu Wizara ya Maendeleo ya
Jamii Jinsia na Watoto, awali alikuwa Naibu Katibu Mkuu wizara
hiyo.
- Sihaba Nkinga amekuwa Katibu Mkuu
wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, awali alikuwa Naibu
Katibu Mkuu Wizara hiyo.
- Sophia Kaduma amekuwa Katibu Mkuu Wizara ya
Kilimo, Chakula na Ushirika, awali alikuwa Naibu Katibu Mkuu wa Wizara
hiyo.
Balozi Sefue aliongeza kwamba:
- Katibu Mkuu aliyepewa uhamisho
ni Peniel Lyimo ambaye anahamia Ofisi ya
Rais - Ikulu kwenye “Presidential’s Delivery Bureau” kama Naibu
Mtendaji Mkuu mwenye jukumu la kuanzisha na kuongoza Idara ya Mageuzi ya
Kilimo mwanzoni alikuwa Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu.
Makatibu wakuu watakaopangiwa kazi nyingine ni:-
- Sethi Kamuhanda aliyekuwa Katibu Mkuu wa
Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo
- Kijakazi Mtengwa aliyekuwa Katibu Mkuu Wizara
ya Maendeleo ya Jamii Jinsia na Watoto
- Injinia Omari Chambo aliyekuwa Katibu Mkuu
Wizara ya Uchukuzi
Katibu anayestaafu ni Patrick Rutabanzibwa ambaye alikuwa Katibu Mkuu
Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, ambaye sasa amestaafu kwa
hiari.
Aidha, Balozi Sefue alisema Rais Kikwete pia amefanya uteuzi wa Naibu Makatibu
Wakuu wapya na kuwapa uhamisho baadhi yao. Aliiwataja Naibu Makatibu
Wakuu wapya walioteuliwa kuwa ni:-
- Angelina Madete amekuwa
Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Mazingira
- Regina Kikuli amekuwa Naibu Katibu Mkuu Ofisi
ya Waziri Mkuu
- Zuberi Sumataba amekuwa Naibu Katibu Mkuu Ofisi
ya Waziri Mkuu – TAMISEMI, anayeshughulikia suala la elimu
katika ngazi za Serikali za Mitaa
- Edwin Kiliba amekuwa Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu -
TAMISEMI
- Deodatus Mtasiwa amekuwa Naibu Katibu Mkuu
Ofisi ya Waziri Mkuu - TAMISEMI ambaye atashughulikia saula la
afya upande wa Serikali za Mitaa.
- Dk Yamungu Kayandabila amekuwa Naibu Katibu Mkuu Wizara ya
Kilimo, Chakula na Ushirika
- Profesa Adolf Mkenda amekuwa Naibu Katibu Mkuu ya Fedha
anayeshughulikia sera
- Dorothy Mwanyika amekuwa Naibu Katibu Mkuu
Wizara ya Fedha anayeshughulikia Fedha za Nje na Madeni
- Rose Shelukindo amekuwa Naibu Katibu Mkuu
Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa
- Dk Selassie Mayunga amekuwa Naibu Katibu Mkuu Wizara
ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi
- Monica Mwamunyange amekuwa Naibu Katibu Mkuu
Wizara ya Uchukuzi
- Consolata Mgimba amekuwa Naibu Katibu
Mkuu Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi
- Profesa Elisante ole Gabriel Laizer amekuwa Naibu Katibu Mkuu
Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo
- Armantius Msole amekuwa Naibu Katibu Mkuu
Wizara ya Ushirikiano wa Afrika Mashariki
Balozi Sefue aliwataja Naibu Makatibu Wakuu waliopewa uhamisho kuwa ni:-
- John Mngondo ambaye amehamishiwa Wizara ya
Wizara ya Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia ametoka Wizara ya Uchukuzi
katika nafasi hiyo
- Selestine Gesimba amehamishiwa Wizara
ya Maliasili na Utalii, anatoka Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi
- Injinia Ngosi Mwihava anahamia Wizara ya Nishati na Madini
kutokea Ofisi ya Makamu wa Rais
- Maria Bilia amehamia Wizara ya Viwanda na Biashara kutoka
Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi
- Nuru Milao anahamia Wizara ya Maendeleo ya
Jamii, Jinsia na Watoto kutoka Wizara ya Maliasili na Utalii.
|
No comments:
Post a Comment