Monday, June 25, 2012
HISTORIA YA RAIS MPYA WA MISRI MOHAMED MOSRI
Muhammad Morsi Isa' al-Ayyat alizaliwa tarehe 20 mwezi agust mwaka 1951 katika jimbo la Sharqia lililopo kaskazini mashariki mwa nchi hiyo
Mosri alipata elimu yake ya msingi na sekondari katika jimbo hilo ,na kujiunga na elimu ya juu katika chuo kikuu cha Cairo akisomea uhandisi ambapo mwaka 1975 alipata shahada ya kwanza.
Mwaka 1978, Musri alihitimu mafunzo yake ya Uhandisi katika chuo hicho na kupata shahada ya uzamili ambapo alielekea nchini Marekani na kujiunga na chuo kikuu cha kusini mwa Califonia ambapo mwaka 1982 alihitimu mafunzo yake na kupata shahada ya uzamivu.
Musri alihudumu kama profesa msaidizi katika chuo kikuu cha Califonia Northridge tangu mwaka 1982 hadi 1985.
Mwaka 1985 Musri alirejea nchini Misri na kuwa mhadhiri mwandamizi katika chuo kikuu cha Zagazig.
Muhammad Morsi Isa' al-Ayyat amehudumu ndani ya bunge la misri tangu mwaka 2000 hadi mwaka 2005 ambapo alichaguliwa kama mgombea binafsi kufuatia chama chake cha muslimu brotherhood kufungiwa na utawala wa aliyekuwa rais wa zamani wan chi hiyo hosni Mubarak.
Alikuwa mwanachama na miongoni mwa waanzilishi wa chama cha muslimu brotherhood kilicho kilichoshiriki kikamilifu katika kuung’oa ulawala wa hosni mubarak mwaka 2011, ambapo yeye alichaguliwa kuwa mwenyekiti wa kwanza wa chama hicho .
Baada ya Khairat El-Shater kukosa uhalali kuwa kukiongoza chama hicho katika uchaguzi wa urais 2012, Morsi, ambaye awali kuteuliwa kuwa mgombea alilijitokeza kama mgombea mpya wa cha Muslim Brotherhood
Kufuatia duru ya kwanza ya uchaguzi wa urais nchini Misri kupatia bwana musri asilimia 25.5% ya kura kiongozi huyo ametangaza rasmi kama rais tarehe 24, june mwaka 2012 baada ya duru ya pili ya uchaguzi kumpatia kura 13,230,131, sawa na asilimia 51.7% huku mpinzani wake Bw.Shafiq akipata kura 12,347,380, sawa na asili mia 48.27%.
Kazi kubwa ya bwana Musri kuwaunganisha raia wote wan nchi hiyo waliyo gawanyika kwa misingi ya kisiasa na kidini
Hata hivyo pamoja na kuwepo kwa hali hiyo ,mtihani mungine umekuwa ukimkabili kiongozi huyo ni ule wa kurudisha mamlaka zote za rais zilizochukuliwa na utawala wa kijeshi nchini humo ambao tatayari umtoa onyo kali kwa yoyote atakekiuka taratimu na sheria zilizowekwa
Akiashiria kuwa mapinduzi bado yanaendelea hadi pale yatakapofikiwa malengo yote ya wananchi amesema, umoja wa kitaifa ni muhimu sana katika kipindi hiki kwa Wamisri.
Tayari viongozi mbambali ulimwenguni waeendelea kupongeza ushindi huo .
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment