Saturday, June 30, 2012



   WAASI WA KIISLAMU NCHINI MALI WAONYA KUINGILIWA

Makundi ya waasi wa kiislamu nchini Mali yametishia kupambana na nchi yoyote itakayounga mkono jeshi la pamoja  la jumnuiya ya kiuchumi ya afrika magharibi ili kuvamia eneo lao

Kundi la waasi wa Tuareg

Makundi hayo likiwemo lile Ansar Dine lenye mfungamano na kikundi cha kigaidi cha Al-Qaeda yameanzisha sharia za kiislam kaskazini mwa Mali na kushuhudia zikishindwa sheria hizo zikshindwakutekelezeka.

Kundi la waasi wa Ansar Dine

Msemaji wa vuguvugu hilo, Adnan Abu Walid Sahraoui amesema, wapiganaji wake wako tayari kila pembe ya nchi yao ya azawada watashambulia kila nchi itakayotuma jeshi lake kaskazini mwa mwa nchi hiyo 

hatua hiyo inakuja wakati ,Jumuiya ya Kiuchumi ya Nchi za Magharibi mwa Afrika ECOWAS ikimesema inajiandaa kutuma jeshi lake kupambana na makundi ya waasi walioteka eneo la kaskazini mwa Mali na kujitangazia uhuru wa nchi mpya waliyoipa jina la Azawad

Ramani ya Mali ikionesha taifa la jipya la waasi la  AZAWAD




Wakuu wa jumuiya ya kiuchumi ya kanda ya Afrika magharibi walikutana nchini cote d' Ivoire kujadili namna ya kumaliza machafuko na kufikia uamuzi wa kutuma jeshi la watu elfu tatu na mia tatu.

Viongozi wa ECOWS

Wakati huohuo kwa upande wa kundi la kiislamu la MUJAO, limedai kuhusika na shambulizi la ijumaa huko Algeria ambapo walishambulia makao makuu ya polisi nchini humo na kuua mtu mmoja na watatu kujeruhiwa.

No comments:

Post a Comment

AddThis

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...