Monday, June 25, 2012

IDADI YA VIFO VINAVYOTOKANA NA SHAMBULIO  YAONGEZEKA KENYA


Idadi ya vifo vilivyotokana na shambulizi la guruneti katika baa moja mjini Mombasa nchini Kenya imeongezeka na kufikia watu watatu leo Jumatatu na majeruhi thelathini bado wanapatiwa matibabu hospitalini, ikiwa ni pigo jipya katika juhudi za serikali katika kuimarisha usalama wa taifa na kufufua utalii.

Msemaji wa shirika la msalaba mwekundu nchini Kenya Nelly Muluka amesema kuwa watu wawili wamefariki wakiwa Hospitalini na mmoja amefariki mapema katika eneo la tukio.
 

Hapo awali polisi walisema kuwa mtu mmoja amefariki katika mlipuko uliotokea kwenye bar ya Jericho wilayani Mishomoroni, wakati mashabiki wa soka walipokuwa wakitazama robo fainali ya mashindano ya Euro 2012 kati ya Uingereza na Italia.

Hivi karibuni katika mfululizo wa mashambulizi hayo katika taifa hilo la Afrika Mashariki, kundi la waasi wa kiislam kutoka Somalia la al shiabaab linadaiwa huenda limehusika na shambulio hilo ambalo limetokea baada ya kutolewa kwa tahadhari maalum kwa wageni ambao walitaka kusafiri nchini Kenya.

1 comment:

AddThis

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...