Waziri
wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Prof. Anna Tibaijuka
akiwasalimia wakazi wa kata ya Bunju na Wazo mara baada ya kuwasili
katika eneo hilo kwa lengo la kuzungumza nao ili kutafuta suluhisho la kudumu la mgogoro wa ardhi kati yao na kiwanda cha Saruji cha Twiga jana jioni.
Waziri
wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Prof. Anna Tibaijuka akiongea
katika mkutano wa hadhara na maelfu ya wakazi wa kata ya Wazo na Bunju
waliojitokeza kufuatilia maendeleo ya mgogoro wa ardhi kati yao na
Kiwanda cha Twiga Cement ambapo pamoja na mambo mengine amewahakikishia
wakazi hao kuwa mgogoro huo utapatiwa ufumbuzi wa kudumu na kuwaomba
kutoa ushirikiano kwake
Diwani
wa eneo la Bunju na Wazo Sharif Exavery Majisafi akiongea na wananchi
kabla ya kumkaribisha Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi
Prof. Anna Tibaijuka kuzungumza nao.
Waziri
wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Prof. Anna Tibaijuka (kulia)
akiongea na Mkurugenzi mtendaji wa kiwanda cha Saruji cha Twiga (Twiga
Cement) Bw.Pascal Lessoinne (kushoto) mara baada ya mkurugenzi huyo
kutoa taarifa fupi ya maendeleo ya kiwanda hicho na hali ya mvutano wa
muda mrefu wa umiliki wa maeneo baina ya wakazi wa kata za Bunju na Wazo
jijini Dar es salaam.
|
No comments:
Post a Comment