Wednesday, December 5, 2012

AJALI YA GARI IRINGA, YAUWA WATU 6 WA FAMILIA MOJA

Gari lililopata ajali la Rav 4 T 770 BNP eneo la Tanzangozi, Iringa lililokua likiendeshwa na Bw. Ezekiel Mwaiteleke(Marehemu) majira ya saa sita na nusu mchana na kusababisha vifo vya watu watano wa familia moja papo hapo December 4, 2012

 Baadhi ya kina mama wasamaria wema wa Tanzangozi Iringa wakijaribu kumpepelea mmoja ya majeruhi wa ajali iliyotokea December 4, 2012 huko Tanangozi, Iringa likihusisha Toyota Rav 4 T 770 BMP lililoingia nyuma ya Trailer T 566 BNQ ambapo watu watano wa familia moja waliokua wakitokea Dar kwenda Mbeya walifariki papo hapo

Gari aina ya Scania lenye cabin # T 840 BST likiwa na Trailer # T 566 BNQ likiwa limegongwa kwa nyuma na Toyota Rav 4 T 770 BNP huko Tanangozi, Iringa na kusababisha vifo vya watu watano wa familia moja papo hapo

 Watu sita wamefariki dunia katika ajali mbaya ya gari  iliyotokea mkoa wa  Iringa mapema siku  ya  jumatano

Ajali hiyo imetokea katika eneo la Tanangozi wilaya ya Iringa kwenye kizuizi cha barabara cha mafundi wa kutengeneza barabara kuu ya Iringa -Mafinga mkoani Iringa mida ya saa nane mchana

Kwa mujibu wa mashuda wa tukio hilo chanzo cha ajali hiyo ni dereva wa gari dogo aina ya Rav 4 lenye namba za usajili T 770 BMP kuliparamia lori lenye tela kwa nyuma. 

Katika ajali hiyo abiria wote wanne akiwemo baba na mama wa watoto wawili waliokuwemo katika gari hiyo wamefariki papo hapo

Majina ya waliokufa ni pamoja na Ezekiel Mwaiteleke ambaye ni dereva wa gari hilo na baba wa familia hiyo ,mkewe Grace Mwaiteleke ,mtoto Kelvin Mwaiteleke (2),Happy Mwandike na mfanyakazi wao wa ndani aliyefahamika kwa jina la Linda Ezekiel huku majeruhi katika ajali hiyo ni mmoja na amekimbizwa Hospital ya mkoa wa Iringa.

 

 

 

 


No comments:

Post a Comment

AddThis

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...