Taarifa kutoka nchini Uganda zinaeleza
kuwa, shughuli za uokoaji zinaendelea katika eneo la mashariki mwa nchi hiyo ambako
vijiji vitatu vimedaiwa kufunikwa na udongo, kufuatia maporomoka yaliyolikumkumba
eneo la Bududa nchini humo
Shirika la msalaba mwekundu nchini
Uganda limethibitisha kuwa zaidi ya watu
kumi na wanane wamefariki dunia katika maporomoko hayo.wakati shughuliza
kuwatafuta mamia ya watu walionasa zikiendelea
Baadhi ya wananchi wa Uganda wakiwa sehemu ya maporomoko |
ijiji visivyopungua 11 vimefunikwa na
matope na majabali mazito na hivyo kukumbushia maporomoko mengine ya udongo
yaliyoyakumba maeneo hayo mwezi Machi 2010 na Agosti mwaka jana.
Mwaka 2010, maporomoko mengine ya ardhi yalitokea
katika wilaya hiyo ya Bududa, na kuwauza zaidi ya watu mia tatu.
Maporomoko
hayo ya udongo yadaiwa kutokea kufuatia
kunyesha kwa mvua kubwa
Eneo
hilo linazungukwa na miinuko pamoja na mabonde, kando kando ya mlima Elgon, na
hupokea mvua kubwa katika msimu wa masika.
baadhi ya nyumba zilizokumbwa na maporomoko hayo |
Serikali ya Uganda imekuwa ikiwaimewashauri
wakazi katika maeneo hayo kuhamia maeneo salama lakini wengi wamekataa kufanya
hivyo wakihofia kupoteza mashamba yao yenye rotuba.
wananchi wa uganda katika eneo la maporomoko huko wilaya ya Baduda |
Hata hivyo Serikali ya Uganda inatarajiwa
kutoa taarifa kamili kuhusu janga hilo huku ikisema kuwa itahakikisha kuwa
familia zilizoathirika zinapata msaada wa kutosha''
No comments:
Post a Comment