![]() |
RAIS Jakaya Kikwete
amewapandisha vyeo maofisa wakuu kutoka cheo cha Meja Jenerali kuwa Luteni
Jenerali kuanzia Novemba 21,mwaka huu.
Kwa mujibu ya taarifa iliyotolewa na Kurugenzi
ya Habari na Uhusiano ya Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), inaeleza kuwa
maofisa wakuu waliopandishwa cheo ni Meja Jenerali, Sylvester Chacha Ryoba
ambaye ni Mkurugenzi wa Kitengo cha Maafa ofisi ya Waziri Mkuu kuwa Luteni
Jenerali.
Mwingine ni Meja Jenerali, Charles Lawrance Makakala ambaye ni Mkuu wa Chuo cha Taifa cha Ulinzi.
Rais Kikwete na Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi, Jenerali Davis Mwamunyange amewapongeza wakuu hao.
Mwingine ni Meja Jenerali, Charles Lawrance Makakala ambaye ni Mkuu wa Chuo cha Taifa cha Ulinzi.
Rais Kikwete na Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi, Jenerali Davis Mwamunyange amewapongeza wakuu hao.
Wakati huohuo, Rais Jakaya Kikwete kesho anatarajia kufanya ziara ya siku moja mjini Rufiji, licha ya mambo mengine atahutubia mkutano wa hadhara mjini Ikwiriri.
Akizungumza jana kwenye Baraza la Madiwani, Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Rufiji, Leonard Rwegasira alisema Rais Kikwete atapokelewa mpakani mwa wilaya ya Kilwa na Rufiji, eneo la Malendego.
Rwegasira alisema wananchi wa Rufiji wametakiwa kujitokeza kwa wingi kumpokea kiongozi huyo atakapoingia wilayani hapa ikiwa ni ziara yake ya kwanza tangu kumalizika kwa Uchaguzi Mwaka 2010.
Hata hivyo, Rwegasira aliwataka madiwani kuwajulisha wananchi kushiriki kumpokea.
No comments:
Post a Comment