Friday, November 23, 2012



RAIS KIKWETE AKUTANA NA VIONGOZI WA SEKTA YA AFYA IKULU, APOKEA CHETI CHA HESHIMA CHA  UDAKTARI - MUHAS

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akipokea  toka kwa Makamu Mkuu wa Chuo cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili Prof. Ephata Kaaya Cheti cha Udaktari wa Public Health (Honoris Causa), kufuatia Shahada aliyotunukiwa na Chuo hicho mwaka  2010 kwa Kutambua mchango wa Rais Kikwete katika kuendeleza Sekta ya Afya nchini. Sherehe hiyo fupi ilifanyika leo Novermba 23, 2012 Ikulu jijini Dar es salaam. 

Makamu Mkuu wa Chuo cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili Prof. Ephata Kaaya akisoma risala kabla ya kumkabidhi Rais Kikwete Cheti cha Udaktari wa Public Health (Honoris Causa), kufuatia Shahada aliyotunukiwa na Chuo Desemba mwaka 2010 kwa Kutambua mchango wa Rais Kikwete katika kuendeleza Sekta ya Afya nchini leo Novermba 23, 2012 Ikulu jijini Dar es salaam..   

No comments:

Post a Comment

AddThis

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...