MAHAKAMA
YAAMURU MADIWANI WATANO KULIPA CHADEMA SH15 MILIONI
MAHAKAMA
ya Hakimu Mkazi Mkoa wa Arusha, imewaamuru madiwani watano waliotimuliwa
Chadema kulipa gharama za kesi waliyokuwa wamefungua kupinga kufukuzwa
uanachama, vinginevyo watapelekwa magereza.
Hakimu
Mkazi Mfawidhi wa Mahakama hiyo, Charles Magesa alitoa hukumu hiyo jana baada
ya Chadema kushinda kesi hiyo.
Hakimu
Magesa alisema madiwani hao wanapaswa kulipa Sh15 milioni ndani ya miezi
miwili, wakishindwa watapelekwa gerezani.
Madiwani
hao ni Estomih Mallah (aliyekuwa Naibu Meya ya Manispaa ya Arusha kipindi
hicho), John Bayo aliyekuwa Diwani wa Elerai, Reuben Ngowi (Themi), Charles
Mpanda (Kaloleni) na Rehema Mohamed aliyekuwa Diwani wa Viti Maalumu.
Pia,
katika kesi hiyo ya madai Chadema walikuwa wakiwakilishwa na Wakili Method
Kimomogoro, wakati wadaiwa hao walikuwa wakijitetea wenyewe baada ya aliyekuwa
wakili wao kujitoa.
Akisoma
uamuzi huo, Hakimu Magesa alisema baada ya mahakama kupitia hoja za pande zote,
imeona wadaiwa hao wanapaswa kulipa zaidi ya Sh15.1 milioni, kila mmoja
anatakiwa kulipa zaidi ya Sh3.2 milioni katika kipindi kisichozidi miezi
miwili.
Awali,
kulikuwa na mvutano kati ya wadaiwa hao jambo lililosababisha kesi hiyo
kusikilizwa kwa kipindi kirefu ambapo walitakiwa kueleza mahakama hiyo sababu
ya kutokupelekwa gerezani, huku kila mmoja akitamka kiwango cha fedha ambacho
angeweza kulipa kwa mwezi.
Kwa
upande wake, Ngowi alisema ana uwezo wa kulipa Sh25,000 kwa mwezi, Mpanda
Sh20,000, Mallah Sh20,000, Rehema Sh15,000 na Bayo Sh15,000 kwa mwezi bila
kuonyesha mchanganuo wa kipato chao, jambo lililopingwa vikali na Wakili
Kimomogoro kwamba kiwango hicho ni kidogo.
No comments:
Post a Comment