TASNIA ya filamu nchini Tanzania, imefikwa na msiba mwingine Mkubwa wa
Msanii wa Filamu, John Stephano Maganga aliyefariki jana katika Hospitali ya
Muhimbili baada ya kuugua kwa muda mfupi.
Kwa mujibu wa taarifa kutoka kwa viongozi wa Wasanii zinasema kuwa
Mipango ya mazishi inafanyika Nyumbani kwao Mwananyama A jirani na Kopakabana
Bar jijini Dar es Salaam.
Marehemu John anaetarajiwa kuzikwa siku ya jumanne Makaburi ya Kinondoni
Dar es Salaam, alianza kujiingiza katika sanaa ya uigizaji mwaka 2001 chini
Thea na Deo Shija na ilipofika mwaka 2008 alianza kuigiza filamu na hadi mauti
yanamfika alikuwa njiani kutoa Filamu yake.
Aidha Wasanii wote wanataarifiwa kufika katika Kikao Maalum Nyumbani kwa
John Stephan oleo Saa tisa alasiri kwaajili ya kupanga mikakati, ya mazishi.
No comments:
Post a Comment