VIJANA WAAFRIKA WAASWA KUWA
CHACHU YA MAENDELEO
MEYA WA ILALA JERRY SILAA AKIWA NA KIONGOZI WA UJUMBE WA MSUMBIJI LOPEZ TEMBE NDELANA |
Vijana
katika nchi za Afrika wameaswa kuwa chachu ya mabadiliko yatakayosaidia kuleta
maendeleo endelevu kwa ustawi wa wananchi wao
Ushauri
huo umetolewa na kaimu katibu mkuu wa chama cha Mapinduzi ccm ambaye pia ni
meya wa manispaa ya Ilala na mjumbe wa halmashauri kuu ya chama hicho Jerry
Silaa wakati akiwapokea vijana 56 wanachama wa chama kinachotwala nchini
Msumbiji cha FRELIMO waliokuja nchini ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya miaka
50 tangu chama hicho kianzishwe
Kaimu
katibu mkuu huyo amesema vijana wa nchi za Afrika wanao wajibu wa kuhakikisha
wanasaidia harakati za serikali zao katika kuwaletea wananchi maendeleo kwa
kufanya kazi kwa bidii na kushiriki shughuli za vyama zenye lengo la kuleta
umoja na mshikamano
Kwa upande wake kiongozi wa msafara huo wa
vijana 56 kutoka mikoa yote nchini Msumbiji balozi Lopez Tembe Ndelana
ambaye ni mmoja wa waasisi wa vuguvugu
la uhuru wan chi hiyo aliyeshiriki katika harakati hizo zilizoanzi ahapa nchini
amewashukuru watanzania ambao walishirikiana na wananchi wa Msumbiji katika
kujikomboa.
Msumbiji
ilipata uhuru wake mwaka 1975 ikiwa chini ya chama cha FRELIMO ambacho
kimefikisha miaka 50 jana Jumapili
No comments:
Post a Comment