BAADA YA SAKATA LA UBAGUZI WA RANGI HATMAYE JOHN TERRY AACHIA NGAZI KATIKA SOKA LA KIMATAIFA.
Terry, ambaye ni mlinzi
wa klabu ya Chelsea, na mwenye umri wa miaka 31, alitangazwa na mahakama ya
Westminster mjini London mwezi Julai kwamba hana hatia ya kutumia matamshi ya
ubaguzi wa rangi dhidi ya Anton Ferdinand, tukio ambalo lilifanyika katika
mechi ya ligi kuu ya Premier.
Terry alimpigia simu
meneja wa England, Roy Hodgson, kabla ya kuwasilisha wazi taarifa yake Jumapili
jioni.
Alisema: “Kuendelea
kufuatia mashtaka dhidi yangu wakati mahakama tayari imeshafanya uamuzi na
kupata sina hatia….hayo hayanipi nafasi kutimiza wajibu wangu.”
No comments:
Post a Comment