MBUNGE WA VITI MAALUM KUSHOTO {CHADEMA} PHILIPA MTURANO |
JAMII
YATAKIWA KUWAUNGA MKONO WAALIMU KATIKA MALEZI.
Jamii
imetakiwa kuwajibika kwa kuwaunga mkono walimu katika malezi ya wanafunzi ili
waweze kupata mafanikio katika masomo.
Akizungumza
wakati wa mahafali ya kidato cha NNE Shule ya sekondari Magnusi,Mbunge wa viti
maalum kupitia tiketi ya Chama Cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA Phillipa
Mturano amesema walezi wamekuwa na tabia ya kuwaachia mzigo waalimu pekee.
Pia mbunge huyo amesisitiza wananchi kuchangia
gharama za uendeshaji wa shule ili ziweze kukidhi mahitaji na malengo yaliyokusudiwa
badala ya kuachia mzigo huo kwa serikali.
Katika
hatua nyingine Bi Phillipa Mturano amewasihi
waalimu kutojihusisha na migomo bali wafuate taratibu za mazungumzo na
serikali ili iweze kuwatimizia maslahi yao.
No comments:
Post a Comment