Saturday, September 8, 2012

TETEMEKO LA ARDHI LASABABISHA VIFO VYA WATU 80 KUSINI MWA CHINA


Tetemeko la ardhi lililotokea jana mchana huko Yiliang, kusini mwa China limesababisha vifo vya watu 80 na wengine zaidi ya laki 7.4 kuathiriwa.

Tetemeko hilo lenye nguvu ya 5.7 kwenye kipimo cha Richtar lilitokea katika sehemu ya mabonde yenye hali duni ya maendeleo, na kuharibu vibaya miundo mbinu ya barabara na mawasiliano ya simu. 

Hivyo kuchelewesha kazi ya kukusanya habari kuhusu vifo na majeruhi pamoja na hasara za mali zilizosababishwa na maafa hayo. 

Waziri mkuu wa China amefika katika sehemu hiyo kuongoza kazi ya uokoaji na kukabiliana na maafa. 




No comments:

Post a Comment

AddThis

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...