Watu wameanza kufikiria ni fundisho gani linalotakiwa kupata kutokana na tukio hilo pamoja na athari zake kwa siasa nchini Afrika Kusini.
Wengi waliofanya mgomo ni wale wanaofanya kazi ya kupasua mwamba, ambayo ni kazi muhimu zaidi katika mgodi wa madini ya platinum, lakini pia ni kazi ngumu na hatari zaidi, kwani wachimba madini wanaweza kufa au kujeruhiwa kutokana na maporomoko ya udongo au mwamba unaweza kuwaangukia wakati wowote.
Matatizo mengi yanawakabili, kama vile ukosefu wa maji safi na salama ya kunywa, nymba bora za kuishi pamoja na kupanda kwa mfululizo kwa bei za bidhaa nchini Afrika Kusini.
Mbali na kampuni ya Lonmin kukataa kutimiza madai yao ya kuongezewa mishahara, kinachowakasirisha wachimba madini hao ni pengo kubwa kati ya matarjiri na maskini.
Wastani wa pato la taifa GDP nchini Afrika Kusini limefikia dola 8,000 za kimarekani, lakini karibu asilimia 40 ya watu wake wanaishi kwa chini ya dola 3 kwa siku.
Pengo hilo kubwa linaonekana zaidi katika sekta ya madini.
Chama cha wafanyakazi wa nigodini ni mwenza wa muda mrefu wa chama tawala, ANC, na mwenyekiti wa zamani wa chama hicho cha wafanyakazi Cyril Ramaphosa ni mtu maarufu sana ndani ya ANC, Ramaphosa pia ni mjumbe wa bodi ya kampuni ya Lonmin, na ni miongoni mwa watu matajiri zaidi nchini Afrika Kusini.
Katika wiki mbili zilizofuata, wawekezaji wa nchi za nje waliuza dhamana za Afrika Kusini zenye thamani ya dola milioni 373. Nchi za China na Brazil, Afrika Kusini imefanikiwa kuvutia mitaji kutoka nchi za nje. Lakini baada ya tukio hilo la umwagaji damu, wawekezaji wanachukua tahadhari kubwa kabla ya kuamua kuwekeza nchini Afrika Kusini.
No comments:
Post a Comment