SIMU SILAHA TOSHA YA KUKAMATA MWIZI GHANA
Herman Chinery-Hesse Mvumbuzi wa programme |
Mvuumbuzi wa programu hii ya Kighana
Herman Chinery-Hesse alitaka kuchukua hatua dhidi ya matukio ya ujambazi wa
kutumia silaha mjini Accra. Ndivyo alivyokuja na programu hii ya "Hei
Julor" au "Ewe mwizi" kwa lugha ya wenyeji wa mji huo.
"Hei Julor" ni programu ya
mfumo wa usalama inayotumiwa katika simu ambapo mtu anaweza kutuma ujumbe mtupu
kutoka kwenye simu zaidi ya tano zilizosajiliwa katika eneo, pale makaazi ya
mtu au biashara yanapovamiwa.
Hatua hii inasababisha kutumwa kikosi
cha waokoaji kutoka kampuni binafsi ya ulinzi, na wakati huo huo watu wengine
kumi wakiwemo majirani na marafiki wanapata ujumbe huo na wanaweza kufika
haraka nyumbani kwa mhusika ili kumsaidia.
Huduma hii ya Hei Julor ilizinduliwa
chini ya mwaka moja nyuma, wakati wa vuguvugu la mageuzi katika mataifa ya
kiarabu na wakati ambapo maandamano ya vrugu yalikuwa yanafanyika nchini
Uingereza.
Katika matukio yote mawili, teknolojia ya simu za mkononi
kama vile ujumbe wa Blackberry au BBM ulikuwa ukitumika kuratibu shughuli.
Chinery-hesse, ambaye amepewa jina la baba wa teknolojia barani Afrika
anakumbuka jinsi yeye na marafiki zake walivyokuja na wazo la "Hei
Julor."
"Tulikuwa tunafuatilia maandamano
katika nchi za kiarabu and nchini Uingereza kupitia redio mchana moja na
ikatujia akilini kuwa walikuwa wakitumia BBM kuratibu maandamano hayo. laazima
itakuwa na manufaa makubwa kwa jamii yetu, katika utamaduni wetu au nchi yetu.
Na kwa sababu hiyo, tulikuja na wazo la "Hei Julor."
Haikuwachukulia muda Chinery-Hesse na
marafiki zake wanaofanya kazi katika kampuni ya programu za kompyuta ya
"Softribe" kuweka mawazo hayo katika vitendo.
"Tumekuwa wataalamu kwa vile hii
ndiyo kazi tunayoifanya kazini kwetu, kwa hiyo tulikuwa na vifa vyote
vinavyohitajika. Tulikaa ofisini, tukamualika kila moja kuhudhuria kikao na
kujadili namna ya kuja na huduma ambayo kila moja angeweza kuipata kwa bei nafuu
na kuizuia Ghana kuwa taifa la wahalifu." Anasema Chinery-Hesse.
No comments:
Post a Comment