Tuesday, September 18, 2012



 
Proscovia Alengot Oromait  amekuwa mbunge wa kwanza  Barani  Afrika kuchaguliwa akiwa na umri mdogo  zaidi nchini Uganda ,kufuatia kifo cha baba yake Michael Oromait aliyekuwa mwaklishi wa jimbo la Usuk nchini humo 

Proscovia Michael Alengot Oromait  akiwa na umri wa miaka 19, ameshinda katika uchaguzi  mdogo  uliofanyika katika jimbo LA Usuk   kwa ticket ya chama tawala cha Uganda National Resistance  Movement  NRM 
 

Kwa mujibu wa matokeo ya uchaguzi mdogo ulilofanyika juma  lililopita  msichana huyu ameibuka kidedea kwa  kupata kura  kumi na moja elfu na  hamsin na tisa  na kufanikiwa kuchukua nafasi hiyo baaada ya kuwashinda wagombea nane  waliokuwa wakiwania nafasi hiyo 
 


Alengot  anachukuwa nafasi  ya baba yake Michael Oromait,  aliyefariuki dunia  mwezi july mwaka huu baada ya afya yake  kusumbuliwa na maradhi  kwa muda mrefu
Mwanada huyo alikuwa akichuana na  Charles Ojok Olenymgombea binafsi aliyepata kura  5,329  huku mgombea wa chama kikuu cha upinzani FDC's Charles Okure akipata 2,725.
 
Anton Abele raia wa sweedeni
wa mujibu wa rekodi zilizopo  ,mwanada huyu anachukua nafasi ya tatu kwa kuwa mbunge mwenye umri mdogo  duniani  baada ya Anton Abele  raia wa sweedeni   kuingia bungeni akiwa na umri wa miaka 18 ,akifuatiwa na raia wa Canada Pierre- Luc Dusseault kuchaguliwa akiwa na umri wa miaka 19  mwaka jana.
raia wa Canada Pierre- Luc Dusseault


No comments:

Post a Comment

AddThis

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...