MANISPAA YA
KINONDONI INADAIWA KIASI CHA SHILINGI BILIONI
8 KUFUATIA KUVUNJA MAKAZI YA WANANCHI BILA KUFUATA TARATIBU ZA KISHERIA
Manispaa ya kinondoni jiji Dar es salaam inadaiwa kiasi cha shilingi bilioni nane na wakazi wa
maeneo hayo kufuatia kuvunjwa kwa maeneo yao bila ya kufuata utaratibu kutoka
serikalini
Hayo yamesemwa September 18 mwaka huu na
mstahik Meya wa manispaa hiyo Bw Yusuph
Mwenda alipokuwa akijibu hoja mbalimbali zilizokuwa zikitolewa na madiwani wa
manispaa hiyo katika kikao chao cha
kawaida cha kujadili mambo mbalimali ikiwemo suala la uvamizi wa maeneo ya wazi
Yusuph Mwenda Mstahik meya Manispaa ya Kinondoni |
Bw. Mwenda amesema kiasi hicho cha fedha kinachodaiwa
kimesababishwa na baadhi ya watendaji wa kata na manispaa kuvamia maeneo ya
wakazi bila ya kufuata taratibukutoka ngazi za juua
Amesema kitendo hicho
kimemsikitisha na watendaji hao
wanapaswa kuwajibishwa ili iwe fundisho kwa watendaji wengine wenye tabia kama
hiyo .
Hivyo meya huyo amefafanua kwamba bado kumekuwepo na tabia ya baadhi ya
watu wanaoendelea kujimilikisha kiholela
maeneo ya serikali ambayo ni maeneo ya wazi
kinyume cha sheria ,hivyo amewataka watu wa namna hiyo waliovamia maeneo
ya Kimara, Mwagwepande, Magomeni Sinza kuhama mara moja
Kwa upande wake mkurugenzi wa manispaa hiyo Bw .Frutunatus Fuema
amesema mwishoni mwa mwaka huu manispaa hiyo itachukuwa hatua,ya kuweka alama
katika maeneo yaliyotengwa ili serikali
iweze kujua maeneo yake.
Zoezi la bomboa bomoa manispaa ya Kinondoni |
No comments:
Post a Comment