![]() |
Chama cha wanasheria Tanzania bara kimemtaka
raisi wa jamuhuri ya muungano wa Tanzania DK Jakaya kikwete kuchunguza baadhi
ya tuhuma zinazowakabili baadhi ya
majaji katika mahakama mbali mbali nchini kufuatia tuhuma alizo zito mbunge
Tundu Lissu katika bunge lililo pita
Bunge la jamuhuri ya muungano wa Tanzania ni
moja ya muhimili muhimu kwa maendeleo ya wananchi ambapo wabunge hukutana na
kujadili masuala mbali mbali yanayo wahusu wananchi wao katika Nyanja mbali
mbali ili kuyapitia ufumbuzi licha ya kuwa ndani ya mijadala hiyo mambo mengi
huibuka zikiwemo kashfa na tuhumha kwa baadhi ya viongozi kama ambavyo katika
bunge lililopita yaliweza kujitokezo
Miongoni mwa tuhuma zilizojitokeza katika
msimu wa bunge uliopita ni pamoja alizo zitoa mbunge wa singida mashariki ambaye ni mnadhimu mkuu
wa kambi rasmi ya upinzani bungeni Tundu
Lissu kuwatuhumu baadhi ya majaji katika baadhi ya mahakama hapa kuwa
wameteuliwa wakiwa hawana sifa zinzotakiwa kwa majaji

Tanzania ni nchi ya kidemokrasia iliyopata
uhuru tangu mwaka 1961 na ni nchi inayoaamika kuwa ni amani kutokana na
historia yake na kila mwanachi ana haki ya kuishi na kwa mujibu wa ibara ya 26
ya katiba ya jamuhuri ya muungano kila mtu ana wajibu wa kutii na kuheshimu
sheria za nchi.
No comments:
Post a Comment