Katika
kuadhimisha siku hiyo hapa Tanzania, shughuli mbalimbali za uelimishaji umma
kuhusu usalama wa usafiri majini zitafanyika kama sehemu ya maadhimisho
ambapo kutakuwa na maonesho ya shughuli zinazofanywa na taasisi
zinazojihusisha na usafiri wa majini yatakayofanyika kuanzia tarehe 26 – 27
Septemba, 2012 katika Viwanja vya Karimjee.
Taasisi
na makampuni yatakayoshiriki maonesho ni pamoja na Wizara ya Uchukuzi,
Mamlaka ya Udhibiti Usafiri wa Nchi Kavu na Majini (SUMATRA), Mamlaka ya
Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA), Chuo cha Bahari cha Dar es Salaam(DMI),
Kilimanjaro Marine Services na Songoro Marine Services.
Aidha SUMATRA imeandaa mkutano wa wadau ambapo itatumia fursa hiyo
kuwasilisha kwa wadau rasimu za kanuni za usalama wa usafiri wa majini.
Mkutano huo utafanyika katika ukumbi wa Mikutano wa Karimjee tarehe 27
Septemba, 2012 kuanzia saa 3.30 asubuhi.
Maadhimisho ya Siku ya Bahari yanatarajiwa kuzinduliwa rasmi na Waziri wa
Uchukuzi, Mheshimiwa Dk Harrison Mwakyembe (MB) tarehe 25 Septemba, 2012.
Wadau na wananchi wote mnakaribishwa katika viwanja vya Karimjee ili kupata
elimu na kujionea juhudi za Serikali na baadhi ya makampuni ya usafiri wa
majini katika kuimarisha usalama wa vyombo vya majini.
|
No comments:
Post a Comment