JE DHIMA YA KUWA NA
MFUMO WA VYAMA VINGI TANZANIA INAIELEWEKA?
Tangu mwaka 1992 tanzania ilipoanza rasmi mfumo wa vyama vingi vya siasa, hali imekuwa ikizidi kubadilika siku hadi siku na hii inatokana na ukweli kwamba mwitikio wa wananchi umekuwa ukizidi kukua kila iitwapo leo.
Tangu chaguzi ya kwanza ya vyama vingi mwaka 1995, kumekuwa na
ripoti mbalimbali za ukiukwaji wa haki za binadamu ambapo rapsha rapsha za hapa
na pale ambazo zimekuwa zikifuatana na milindimo ya risasi imekuwa ikisikika,
Nje kidogo ya kongamano lililoandaliwa na muungano wa asasi za
kirai nchini ambalo limefanyika katika viwanja ya mtandao wa kijinsia Tanzania
TGNP, blog hii imepata fursa ya kuzungumza na baadhi ya wadau pamoja na wasomi
ambao kwanza wanazungumzi milindimo hii ya risasi katika nchi inayotajwa kama
ya kidemocrasia
Wamesema kuwa ni vema watawala wakavitumia vyombo vya ulinzi
na usalama kuwa kuhakikisha vinatimiza wajibu wao wa kulinda usalama wa nchi na
si kuwa vyanzo vya kubomoa amani ya nchini,
Lakini katika nchi ya kidemocrasia kama Tanzania ni yapi
yanapaswa kuzingatiwa ilikuilinda democrasia iliyopo, wanasheria Haloid
sungusia na Albanie marcos
wanazungumza.
Katika duru za kisiasa kwa upande wa kimataifa Tanzania
imekuwa ikijengea heshima kwa kutajwa kama nchi inayojali na kuheshimu misingi
ya kidemocrasia.
No comments:
Post a Comment