Wednesday, September 12, 2012



BREKING NEWSZZZ: Taarifa kutoka mkoa wa Iringa zinaeleza kuwa mtuhumiwa wa mauaji ya aliyekuwa mwandishi wa habari wa kituo cha televisheni cha Channel Ten Daud Mwangosi amefikishwa mahakamani.

Mtuhumiwa huyo amefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mfawidhi ya Wilaya kujibu shitaka lilalomkabili.

Kwa mujibu wa mwendesha mashtaka wa serikali Mkuu Michael Luena, amesema mtuhumiwa huyo ambaye ni askari mwenye namba G2573 Pasificus Cleophace Simoni mwenye umri wa miaka  (23) mkazi wa FFU Iringa, anakabiliwa na shitakala la mauaji ya makusudi.

Amesema mtuhumiwa huyo mnamo Septemba 02mwaka huu katika kijiji cha Nyololo Wilaya ya Mufindi Mkoa wa Iringa alimuua Daudi Mwangosi kwa makusudi kinyume na kifungu cha sheria namba 148 kifungu kidogo 5A.i cha makosa ya jinai.

Mbele ya Hakimu Mkuu Mwandamizi wa mahakama ya hakimu Mfawidhi ya Wilaya Dyness Lyimo mtuhumumiwa hakutakiwa kujibu chochote kwa kuwa mahakama hiyo haiwezi kusikiliza kesi za mauaji.

Kwa mujibu wa kesi za jinai, sheria kifungu 196 kanuni ya adhabu Cap. 16 iliyofanyiwa marejeo mwaka 2002, kinakataza mtuhumiwa wa mauaji ya kukusudia kupewa dhamana.

Mtuhumiwa amerudishwa mahabusu kutokana na kesi yake kukosa dhamana kisheria na kesi hiyo imeahirishwa hadi 26 Septemba mwaka huu itakapotajwa tena mahakamani hapo.

Hata hivyo askari wengi waliompeleka mtuhumiwa huyo wakiwa wamevaa nguo za kiraia walihakikisha kuwa mtuhumiwa huyo hapigwi picha jambalo limewaletea ugumu waandishi waliokuwapo baada ya kusukumwa ovyo kuzuia mtuhumiwa huyo asipigwe picha.


No comments:

Post a Comment

AddThis

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...