NCHIMBI AKUMBANA NA KADHIA KWENYE
MAANDAMANO.
Maaandamano ya
yaliyowajumuisha kwa pamaoja waandishi wakongwe na chipukizi nchini yamefanyika kwa amani na utulivu huku waandishi wakitakiwa kudumisha umoja na mshikamano
Maandamano hayo
yameanzia kituo cha televisheni cha Channel Ten alichokuwa
akifanyia kazi Daudi Mwangosi hadi viwanja vya
jangwani huku wanahabari wakivalia
nguo nyeusi ishara ya kuomboleza
kifo cha mwenzao.
Baada ya kufika
katika viwanja vya Jangwan waziri wa
Mambo ya Ndani, Emmanuel Nchimbi, amekambana na fedhea ambayo haikutarajia wakati alipotimuliwa katika maandamano hayo kwa madai
kuwa hakuna kiongozi yoyote wa serikali aliyealikwa
Wakati wakiwa wamebeba mabango yenye ujumbe tofauti, walipofika mwisho wa
maandamano yao walipigwa na butwaa baada ya kumkuta Waziri Nchimbi akiwa wa
kwanza kufika katika eneo hilo tayari kupokea maandamano.
Wakati Nchimbi akijiandaa kuanza
kuzungumza mbele ya wanahabari, upinzani mkali ulizuka kwa waandishi dhidi ya
kiongozi huyo wa serikali wakitaka aondoke mahala hapo kwani maandamano hayo
yalikuwa hayamuhusu.
‘Atokee.... nchimbi …aondokee.... nchimbi ,
hatumtakiiii.... nani kamleta hapa?" yalikuwa ni baadhi ya maneno
yaliyokuwa wakitolewa kwa sauti kubwa kupinga uwapo wa kiongozi huo
|
Waziri wa mambo ya ndani Emmanuel Nchimbi akilazimika kuondoka kwenye maandamano hayo
|
Mwandishi wa habari mkongwe, ambaye pia ni mwanasheria, Nyaronyo
Kicheere, alisogea mbele ya umati wa waandishi na kusimama jirani na
alipokuwapo waziri Nchimbi na kusema: "Tumeambiwa tunakuja hapa kwa ajili
ya mkutano wa waandishi wa habari na utapokewa na jukwaa la wahariri, inakuwaje
tupokewe na mtu mwingine. Hatumhitaji mtu mwingine hapa, aondoke."
Baada ya kauli hiyo, waziri Nchimbi
aliondoka mahala hapo na kuzua shangwe kubwa kwa waandishi ambao pia
walimsindikiza kwa kumzomea mpaka alipoingia katika gari lake la wizara. Hakuja
na gari lake la waziri.
Wahariri wa vyombo mbalimbali vya
habari walizungumza na kukemea mauaji hayo na bila ya kinyama yanayofanywa
nchini huku wakitaka waliomuua mwandishi huyo wote wachukuliwe hatua za kisheria.
Maandamano hayo pia yamefanyika katika mikoa mingine nchini isipokua mkoa ya Mara na Arusha.
No comments:
Post a Comment