Wednesday, September 12, 2012

 
   RAIS MPYA WA SOMALIA ANUSURIKA KIFO

 Rais mpya wa Somalia Hassan Sheikh Mohamud , amenusurika jaribio la kumuua mjini Mogadishu.

Milipuko miwili imetokea nje la lango la makao ya rais huyo katika hoteli ya Al-Jazeera wakati rais huyo alipokuwa anajiandaa kufanya mkutano na waandishi wa habari.

Taarifa zinasema kuwa waziri wa mambo ya nje wa Kenya Sam Ongeri pia alikuwa katika hoteli hiyo wakati wa shambulizi. 

Hata hivyo wawili hao wamenusurika. Inaarifiwa mtu mmoja ameuawa.

No comments:

Post a Comment

AddThis

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...