VIKAO VYA CCM NEC KUANZA HIVI KARIBUNI
Kikao cha halimashauri kuu ya
Chama Cha Mapinduzi NEC kinatarajia kufanyika kuanzia September 24
mwaka huu mkoani Dodoma, kwa ajili ya kuteuwa majina ya wagombea waliojitokeza
kugombea nafasi mbalimbali ndani ya chama hicho .
Akizungumza na waandishi wa
habari September 18 mwaka huu Katibu wa NEC itikadi na
uenezi bwana Nape Mosses Nauye amesema kikao hicho kitakaa baada ya
kamati kuu kukutana November 22 na 23 mwaka huu.
Amesema September 19 na 20vikao
vya Sekretarieti vitaanza lengo likiwa ni kupitisha majina ya wagombea kwa kuzingatia alama walizoekea katika vikao
vilivyokwisha fanyika.
Kikao hicho cha sekretarieti
kikimalizika,watapeleka mapendekezo yao katika kikao cha kamati ya maadili ambacho kinatatarajiwa kukutana September
21
Katibu huyo amebainisha kuwa vikao
vyote hivyo vitakuwa ni kwaajili ya
kuchuja majina kuanzia kwenye
jumuiya katika ngazi ya kitaifa
wenyeviti na makamu wenyeviti katika ngazi za mkoa na wilaya na kwamba NEC itakapokutana
ndiyo itakayoteuwa majina ya wagombea na baada ya hao ratima ya uchaguzi
itatolewa.
Amesema Viongozi Wakuu Wakitaifa
Wanatarajiwa Kukutana Mwishoni Mwa Mwezi
November Kwa Ajili Ya Uchaguzi Nafasi Ya Mwenyekiti Makamu Mwenyekiti
Katika hatua nyingine bwana Nape amefafua katika kikao hicho kuhusu
uwepo wa mtu asiyejulikana anayetumia
jina lake kuwarubuni baadhi ya wagombea
na kuwaomba fedha na kusema mtu huyo amesajili account yake kwa Jina lake
hivyo kuwaomba wagomea na watanzania kwa ujumla
kutambua kwamba mtu huyo ni tapeli na kwamba hakuna jina la mtu yoyote
litakalopitishwa kwa njia ya rushwa.
No comments:
Post a Comment