Monday, September 24, 2012



DOKTA  MWAKYEMBE ATOA SIKU SABA KWA JESHI LA POLISI KANDA MAALUM YA DARE S SALAM KUTAJA MAJINA YA WATUHUMIWA WA WIZI WA MAFUTA BANDARINI.



Waziri wa uchukuzi -Harrison Mwakyembe

Waziri wa uchukuzi nchini Dokta Harrison  Mwakyembe ametoa siku saba kwa jeshi la polisi kanda maalum  ya dar es  kutaja majina ya  watu  wanaoshukiwa kuhusika na wizi wa mafuta katika bandari ya dar es salaam 

Akizungumza  kupitia shirika la utangazaji la Taifa TBC  jana  Dokta mwakyembe amesema  wizi kama huo  ni jambo linalorudisha nyuma maendelelo ya taifa na  hivyo  halipaswi kutokea katika taifa linalojikongoja kutafuta kujipatia maendeleo yake

Mapema  mwezi huu Waziri wa Uchukuzi Dokta Harrison Mwakyembe aliwasimamisha kazi  Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari-TPA-Ndugu EPHRAIM MGAWE-TPA pamoja na wasaidizi wake wawili ili kupisha uchunguzi wa tuhuma zinazowakabili. 

Wengine waliosimamishwa ni Meneja wa Mafuta ya Ndege Kurasini, Meneja wa JET na Meneja wa Oil Terminal kutokana na tuhuma za kupotea kwa mafuta na kuidanganya serikali kuhusu mafuta masafi na machafu.

Kutokana na kuwasimamisha kazi Wakurugenzi hao Dokta Mwakyembe alimteua Injinia Madeni Kipange kukaimu nafasi ya Mkurugenzi Mkuu wa TPA.Kufuatia tuhuma hizo zinazofanywa Bandarini 

Dokta Mwakyembe aliunda Tume wa ya watu saba kufanya uchunguzi kwa wiki mbili na kumpelekea taarifa ofisini kwake ili kubaini ukweli wa tuhuma hizo zikiwemo za wizi.

Pia aliagiaza  hadi kufikia Septemba Mosi mwaka huu malipo yote yafanyike benki ili kuondoa rushwa na wizi unaofanyika ndani ya
yao kutokana na kutokuwa na inami na watumishi wake hatua inayoifanya serikali kukosa mapato zaidi.



No comments:

Post a Comment

AddThis

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...