Saturday, September 22, 2012



KAULI YA CHADEMA DHIDI YA MSAJILI WA VYMA NCHINI YAJIDHIHIRISHA 
mkurugenzi wa Habari na Uenezi CHADEMA , John Mnyika
Hatmaye  tamko la Chama cha Demokrasia na Maeneleo CHADEMA Kuhusu kutoshiriki kikao chochote kitakachoitishwa na msajili wa vyama vya siasa nchini limejidhihirisha 

Hatua hiyo imeonekana baada ya chama hicho kususia kushiriki katika semina aliyoandaa msajili wa vyama vya siasa nchini John Tendwa iliyohusu amani na usalama nchini 

Chama hicho kimesema hakitashiriki katika semina hiyo  kwa wakati huu kwa madai kuwa kinasubiria hatua za Rais kuhusu mauaji ya kisiasa yaliyotokea katika mikoa mbalimbali nchini.

Akitoa taariofa kwa  vyombo vya habari mkurugenzi wa Habari na Uenezi Chadema, John Mnyika, alamesema chama hicho kimechukua hatua hiyo kikitambua umuhimu wa amani na usalama wa nchi na wajibu wa Jeshi la Polisi pamoja na Vyama vya Siasa katika kukuza demokrasia ya vyama vingi.

Mnyika amesema hatua hiyo imefikiwa kufuatia utendaji dhaifu na wa kipropaganda unaoonyeshwa na Tendwa uliosababisha Kamati Kuu ya Chadema kumtangaza kuwa ni adui wa demokrasia na hafai kuwa katika nafasi aliyo nayo.


“Kamati Kuu iliazimia kuwa pamoja na kuendelea kuheshimu sheria ya vyama vya siasa, Chadema haitashiriki shughuli zozote zitakazosimamiwa na John Tendwa hadi hapo atakapoondolewa katika nafasi yake na kuteuliwa msajili mwingine,” alisema bwana Mnyika .


mnyika amesema  Kamati Kuu ya Chadema ilifanya kikao maalumu Septemba 9 mwaka huu kilichojadili hali ya siasa nchini kufuatia mfululizo wa mauaji yanayofanywa na Jeshi la Polisi katika shughuli za kisiasa za Chadema na mipango ya baadhi ya viongozi wa Serikali ya kudhibiti Vuguvugu la Mabadiliko (M4C) kwa mbinu haramu.

No comments:

Post a Comment

AddThis

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...