OBAMA AKUBALI UTEUZI WA CHAMA CHAKE CHA DEMOCRATIC
Rais
wa Marekani Barack Obama amekubali uteuzi wa chama chake, Democratic, kugombea
muhula wa pili wa Urais.
Katika
hotuba yake Obama amewaomba
raia wa Marekani kuwa na subira huku akisema itachukua muda kupata suluhisho kwa changamoto
zinazoikabili nchi hiyo
Rais Barack Obama wakati wa akiwahutumia wanachama wa chama chake |
.
Ilikuwa
wakati wa hotuba yake kwenye kilele cha mkutano mkuu wa chama hicho, ambao
umefanyika katika mji wa Charlotte, katika jimbo la North Caroline.
Akizungumza
mbele ya wajumbe 6000 katika mkutano huo, Obama amesema katika uchaguzi wa
mwezi Novemba ambao atakuwa akipambana na Mitt Romney wa chama cha Republican,
wamarekani watakuwa na nafasi kubwa ya
kuamua juu ya mielekeo miwili tofauti
kwa Marekani.
Rais
Obama Amekiri
kwamba nchi yake inakabiliwa na changamoto
nyingi za a kiuchumi kiuchumi, huku
akasema changamoto hizo zinaweza kupatiwa ufumbuzi.
'Itachukua
miaka michache mingine kuweza kuukwamua uchumi ambao umekuwa ukiporomoka kwa
miongo kadhaa. Itahitaji juhudi za pamoja, kuwajibika kwa kila mmoja wetu, na
ujasiri kama ule wa Rais Franklin Roosevelt wakati wa mgogoro mkubwa pekee
kuliko huu wa sasa''. Amesema Obama.
Ikiwa
imeasalia miezi miwili kabla ya kufanyika uchaguzi wa mwezi Novemba, Rais Obama
na mpinzani wake Mitt Romney bado wako sambamba katika kura za maoni,
wademocrats wanazinadi sera zao kuhusu masuala ya usalama, haki za wanawake na
mashoga, uokozi wa sekta ya viwanda vya magari na kuuawa kwa Osama bin Laden
kujaribu kumpa msukumo Rais Obama aweze kumpita mpinzani wake.
Rais Barack obama kulia ,kushoto ni rais wa zamani wa Marekani Bil ClintoN |
Barack
Obama ambaye kampeni zake zinamuonyesha kama mtu anayejali zaidi wamarekani wa
kawaida na haki ya kila raia kutimiza ndoto yake, amehitimisha hotuba yake kwa
kuwataka watu wenye maoni kama yake kumuunga mkono.
Amesema,
''Kama una imani katika nchi ambayo inampa haki kila raia, na ambako watu wote
wako sawa mbele ya sheria, basi, naomba kura yako katika uchaguzi wa mwezi
Novemba''.
Maafisa
wa chama cha Democrats wameuchukulia mkutano wao mkuu kuwa wa mafanikio
makubwa, na ambao umeweza kuamsha hamasa ya wapiga kura.
No comments:
Post a Comment