KAMATI KUU YA CHAMA CHA
DEMOKRASIA NA MAENDELEO CHADEMA YATAKA VIONGOZI
WA JESHI LA POLISI NCHINI WAWAJIBIKE
Baada ya kukukutana na kujadili mambo mbali mbali ikiwemo
mwenendo wa siasa hapa nchini pamoja na mauwaji ya raia yaliyotokea hivi karibuni hatmaye ,kwa kauli moja chama hicho
kimwewataka viongozi wa juu wa Jeshi la
polisi kuwajibika
Chama hicho kimesema kuwa ikiwa vingozi hao watashindwa
kuchukuwa hatuo hiyo bas I ni vema raisi
wa jamhuri ya muungano wa Tanzania Dr.
Jakaya Mrisho Kikwete awawajibisha .
Freeman Mbowe Mwenyekiti CHADEMA |
Katika hatua nyingine viongozi
hao wa CHADEMA pia wameazimia kutoshiriki shughuli zitakazosimamiwa na
msajili wa vyama vya siasa nchini John Tendwa kufuatia kauli aliyoitoa hivi
karibuni ya kufuta chama kinachosababisha
mauaji ,hatua ambayo imepingwa vikali na chama hicho .
Chama hicho pia kinataka rais kuunda tume ya kimahakama
itakayochunguza vifo vinavyotokea katika mazingira tete
kukamatwa na kufikishwa mahakamani kwa mkuu jeshi la polisi mkoa wa
Iringa Michael Kamuhanda ,Mkuuu wa kikosi cha kutuliza ghasia mkoa wa Morogoro pamoja na maaskari waliomuua aliyekuwa
mwandishi wa channel Ten Daudi Mwangosi.
Maazimio mengine ni yaliyotolewa na chama hicho ni pamoja na
kuwavua uanachama madiwani wawili
wa chama cha demokrasia na maendeleo CHADEMA mkoa wa Mwanza walioenenda kinyume
na sheria na kanuni za chama hicho
No comments:
Post a Comment