Wednesday, September 5, 2012



       MGOMO WA WAALIMU WAINGIA SIKU YA PILI NCHINI KENYA

Baada ya   serikali Nchini Kenya kuupuuza kilio cha muda mrefu cha waalimu kuhusu  madai ya kutaka kuboreshewa  mazingira ya kazi lakini  pia kutaka nyongeza ya mishaara hatimae walimu wanchi hiyo  wamecharuka nakuamua kusitisha shughuli zao.
Mgomo wa waalimu nchini Kenya

Katika kile kilichoonekana kama ni kuchoshwa na ahadi zisizotekelezeka zinazotolewa na serikali Maelfu ya walimu nchini humo wamenza mgomo usiokuwa na kikomo siku ya jumatatu kwa madai kuwa serikali imekuwa ikipuuza kilio chao.

Licha ya kuwepo kwa agizo la mahakama lililoharamisha mgomo huo ,walimu hao wamekaidi hatua hiyo hali iliyolazimimu Shule nyingi katika miji mikubwa ya Mombasa, Nairobi na Nakuru zikisalia  kufungwa.

Mgomo huu unajiri wakati shule zikifungua kwa muhula wa tatu kitu ambacho walimu hao wanasema sio hoja kwani wamekuwa wakigoma kila muhula wa tatu unapofungua kwa zaidi ya miaka kumi iliyopita wakidai stahiki zao .



Wanasema serikali ya nchi hiyo haina usawa katika suala zima la utoaji wa mishahara kwa wafanyakazi wa umma kwani ni hivi karibuni wauguzi pamoja na wafanyakazi wengine wa umma walipoongezwa mishara baada kupitia hatua hiyo
 Chama cha Walimu nchini Kenya KNUT kimesema walimu hawatorudi kazini hadi pale matakwa yao yatakapotekelezwa.

Walimu wanadai asilimia 300 ya nyongeza ya mishahara pamoja na kutekelezwa makubaliano ya mwaka 1997 yanayoitaka serikali kuongeza marupurupu kwa walimu

Zaidi ya shule  laki mbili na hamisini  za serikali zimefungwa huku zikiathiri mamlion ya wanafunzi

.

No comments:

Post a Comment

AddThis

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...