AL-SENUSSI AKABIDHIWA KWA WATAWALA WA LIBYA
Serikali ya Mauritania imewakabidhi maafisa wa utawala wa Libya aliyekuwa mkuu wa ujasusi nchini humo, Abdullah al-Senuss
Libya inataka kumfungulia mashtaka
bwana Senussi kwa makosa aliyoyafanya chini ya utawala wa hayati Muamar
Gaddafi.
Abdullah al-Senuss |
Mapema mwezi huu rais wa Mauritania,
Mohamed Ould Abdel Aziz alisema kuwa bwana Sanusi aliyekuwa amekimbilia nchini
humo, sharti kwanza akabiliwe na sheria kwa makosa ya kuingia Mauritania
kinyume na sheria.
Senussi alitoroka Libya baada ya
mapinduzi ya mwaka jana ambayo yalimng'oa mamlakani Muammar Gaddafi.
Pia anatakiwa na Ufaransa pamoja na
mahakama ya kimataifa kuhusu haki za bianadamu ICC kwa makosa ya kukiuka haki
za binadamu.
Ripoti za kukabidhiwa kwake kwa
watawala wa Libya, zilitolewa na televisheni ya taifa pamoja na shirika rasmi
la habari la Mauritania.
Kulingana na ripoti,
bwana Senussi alikabidhiwa kwa wajumbe wa Libya walioongozwa na waziri wa
sheria na haki wa nchi hiyo. Lakini hadi sasa bwana Senussi hajulikani aliko
No comments:
Post a Comment