DOS SANTOS KUONDOZA KIPINDI KINGINE CHA MIAKA MITANO ANGOLA
Hatimae chama tawala nchini Angola cha MPLA kinachongozwa na rais Jose eduardo dos Santos kimetangazwa rasmi kuwa kimeshinda uchaguzi uliofanyika nchini humo siku ya jumaa iliyopita.
Hatua hiyo inampa rais dos Santos hatamu ya uongozi wa miaka mingine mitano zaidi kubeba majukumu ya uongozi huo wa ngazi ya juu kabisa katika nchi.
Kutokana na mabadiliko ya katiba ya mwaka 2010 ni kwamba kiongozi wa chama kilichopata kura nyingi zaidi ndie anayepaswa kutawazwa kuwa rais na kiongozi mkuu wa mkuu washughuli za serikali.
Kwa mujibu Taarifailiyotolewa na Tume ya Uchaguzi na kutangazwa katika mji mkuu Luanda imesema kuwa asilimia 75 ya wapiga kura wamekichagua chama cha MPLA kuendelea kuwa chama tawala nchini humo
Chama kikubwa kabisa cha upinzani, UNITA, kilipata asilimia 18 ya kura ambapo Msemaji wa upinzani na waangalizi huru wa uchaguzi huo awali wamelalamikia tume ya uchaguzi kwamba hajaridhishwa kutokana na kuwepo kasoro katika zoezi la uchaguzi huo.
Huu ni uchaguzi wa tatu nchini Angola tangu ipate uhuru wake kutoka kwa Wareno mwaka 1975. Uchaguzi wa mwisho ulifanyika mwaka 2008.
No comments:
Post a Comment