HALI YA WANANCHI WA SYRIA INATISHA ASEMA LAKHDAR BRAHIMI
Lakhdar Brahimi mpatanishi wa mzozo wa syria |
Mpatanishi wa kimataifa wa mzozo wa
Syria,Lakhdar Brahimi ametoa picha ya kutisha ya hali nchini Syria,akiitaja
idadi ya wahanga ni ya "kushtusha" na "maangamizi yasio na
kifani "yaliyosababishwa na vita nchini humo
Katika wakati ambapo mzozo wa Syria
unaingia katika mwezi wa 18,bila ya kuwepo matumaini ya kuupatia
ufumbuzi,matumizi ya nguvu yanazidi makali-pekee hii leo watu wasiopungua 20
wameuwawa jeshi la serikali lilipouhujumu mji wa Aleppo,walikopiga kambi
waasi,zaidi ya mwezi mmoja uliopita.
Katika hotuba yake ya kwanza mbele
ya hadhara kuu ya Umoja wa mataifa mjini New-York,tangu alipoanza rasmi
shughuli zake kama mpatanishi wa mzozo wa Syria,Lakhdar Brahimi amezungumzia
ziara anazopanga kufanya hivi karibuni mijini Damascus na Cairo.-
Anahisi ni muhimu kupata uungaji
mkono wa jumuia ya kimataifa ambayo haina msimamo mmoja linapohusika suala la
namna ya kuupatia ufumbuzi mzozo wa Syria;warusi,wachina na wairan-washirika wa
utawala wa Bashar al Assad wakipinga mpango wowote wa kuingiliwa mzozo huo na
mataifa ya kigeni ,huku nchi za magharibi na washirika wao wa kiarabu
wakiwaunga mkono waasi.
"Idadi ya wahanga inamfanya mtu
aduwae,hali inazidi kuwa mbaya" ameonya mwanadiplomasia huyo aliyeshika
nafasi iliyoachwa na Kofi Annan na kufafanua umuhimu wa ushirikiano wa jumuia
ya kimataifa.
Bwana Lkhdar Brahimi ameongeza kusema:"Mustakbal wa Syria
utaamuliwa na wananchi wake wenyewe na sio na wengine.Uungaji mkonmo wa jumuia
ya kimataifa ni jambo la lazima na linalohitajika haraka.Uungaji mkono huo
utaleta tija tu ikiwa wote watakuwa na msimamo mmoja."
Ban Ki-Moonkatibu mkuu wa Umoja wa mataifa |
Nae katibu mkuu wa Umoja wa mataifa
Ban Ki-Moon,akihutubia pia mbele ya hadhara kuu ya Umoja wa mataifa mjini New
York,amezikosoa nchi zinazozipatia silaha pande zinazohasimiana nchini Syria na kutoa wito wa kuwepo mshikamano wa jumuia ya kimataifa ili kuwapatia huduma
za kiutu wakimbizi wa Syria ndani na nje ya nchi hiyo.
Urusi na Iran zinatuhumiwa kuupatia
silaha utawala wa Bashar al Assad huku Saud Arabia na Qatar zikitajwa kuwapatia
silaha waasi.
No comments:
Post a Comment