Wednesday, August 21, 2013

VYUO VIKUU VIFUATAVYO VYATUNUKIWA VYATUNUKIWA HATI IDHINI NA RAIS KIKWETE.


Viongozi wawakilishi wa vyuo mbambali nchini

RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Jakaya Mrisho Kikwete ametunuku Hati Idhini ((University Charter)) kwa vyuo vikuu na vyuo vishiriki 8 baada ya vyuo hivyo kutimiza taratibu zote za uanzishwaji wake hapa nchini.

Vyuo vilivyotunukiwa hati  baada ya kutimiza taratibu zote ni Chuo Kikuu cha Tumaini (TUMA), Chuo Kikuu cha Mtakatifu Agustino (SAUT), Chuo  Kikuu Kishiriki  cha Ruaha (RUCo), Chuo Kikuu  cha Mount Meru (MMU), pamoja na Chuo Kikuu cha Arusha (UoA).

Vyuo vingine vilivyotunukiwa hati hiyo ni Chuo Kikuu Kishiriki cha Tumaini Dar es Salaam (TUDARCo), Taasisi ya Afrika ya Nelson Mandela ya Sayansi  na Teknolojia Arusha (NM-AIST) na Chuo Kikuu cha Sayansi  na Teknolojia Mbeya (MUST).



alisema  vimepiga hatua kubwa ya  kuongeza idadi ya wanafunzi wanaojiandikisha hadi kufikia  laki moja sitini na sita elfu mwaka 2013, ukilinganisha na idadi ya wanafunzi elfu arobaini ya mwaka 2005.

“Idadi kubwa ya wanafunzi pekee haitoshi,ubora wa elimu uzingatiwe . Ikiwemo kupata wakufunzi wengi na wenye sifa  ni lazima sisi wenyewe tuwekeze ndani ili kupata wakufunzi wakutosha katika vyuo vyetu,” alisema Rais Kikwete.

Aidha Rais  Kikwete  alivitaka vyuo hivyo kutekeleza  mkakati wa elimu wa  Matokeo  Makubwa Sasa (Big Results Now)  ipasavyo  ili kuboresha elimu nchini kwa kuimarisha miundombinu  ya  vyuo vikuu nchini.


 Utoaji wa Hati Idhini kwa vyuo vikuu  ni zoezi endelevu linalolenga  kuboresha  kiwango cha utoaji elimu  ya juu nchini  ili kuwezesha wahitimu  kukabiliana na changamoto  za maendeleo  ya taifa letu kwa ujumla.

Mara ya mwisho zoezi hili lilifanyika  tarehe 18 Agosti, 2010 ambapo jumla ya vyuo vikuu na vyuo vishiriki  13 vilitunukiwa Hati Idhini.



No comments:

Post a Comment

AddThis

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...