Tuesday, June 26, 2012


        RWANDA YAENDELEA KUKANUSHA MADAI YA KUWAFADHILI WAASI WA DRC

Serikali ya Rwanda imeendelea kukanusha vikali tuhuma kuusu kuwafadhili waasi wanaopambana na serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo DR wanaoendeleza mapambano mashariki mwa nchi hiyo 

Waziri wa Mambo ya Nje wa Rwanda amesema hayo akiwa katika Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa UN na kusema uzushi na taarifa ambazo zinaihusisha nchi hiyo kufadhili waasi wa DRC hazina ukweli wowote.

Waziri wa mambo ya nje wa Rwanda -Louise Mushikiwabo



amesema serikali yake ipatiwe ushahidi unaodhihirisha wao ndiyo vinara  wa kuwahifadhi waasi wanaopambana na serikaliya Kinshasa kutoka eneo la Mashariki.



Waasi wa DRC Congo.

Mapambano ya mashariki mwa nchi ya Jamuhuri ya demokrasia ya Congo dhidi ya waasi yamechangia adha nyingi kwa wakazi wa maeneo hayo ikiwemo vifo,watu kuyakimbia makazi yao,kukosekana kwa utulivu na hivyo watu kushindwa kuendelea na shughuli za uzalishaji.

Raia wa Congo DRC wakiyakimbia makazi yao kutokana na ghasia baina ya waasi na majshi ya serikal




No comments:

Post a Comment

AddThis

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...