Monday, December 17, 2012

PICHA YA BUNDUKI ALIYO TUMIA ADAM KUFANYIA MAUAJI YA KINYAMA YA WATOTO WA SANDY HOOK SCHOOL


Hii ndiyo bunduki ya aina ya (Bush Master AR 15 assault weapon) aliyo tumia Adam Lanza (20) kutoa roho za watoto wadogo wasio kuwa hata na ufahamu wa ugumu wa maisha na stress zake. 

Adam kabla ya kufika eneo la shule na kufanya unyama huo alianza kumuua mama yake mwenyewe na kisha kuchukua gari la mama yake aliekuwa anaitwa Nancy Lanza (52) na kuliendesha gari hilo hadi shuleni na kufanya unyama wake aliohukusudia. 

Inasemekana ndani ya gari hilo la mama yake kulikuwa na bunduki zingine mbili aina ya Glock 10 mm and a Sig Sauer 9mm. Adam alitoa uai wa mama yake kwa kumpiga kichwani mala 4.

 Na inasemekana mama yake mwenyewe ndo alimfundisha mtoto wake jinsi ya kutumia bunduki hizo masikini kama angelijua wala asinge mfundisha jinsi ya kutumia siraha hizo.

 Hapa chini ni mchoro wa bunduki hiyo aina ya Bushmaster jinsi hilivyo na nguvu na kufikiria kuwa imetumia kutoa roho za watoto wadogo waliyo shutiwa zaidi ya mala tatu mwilini mwao huu ni unyama mwenyezi mungu azilaze pema nyoyo za malaika hao na pole kwa wazazi waliopoteza watoto wao wapendwa, mwenyezi mungu awatie nguvu na imani katika kipindi hiki kigumu. Ameen

 

No comments:

Post a Comment

AddThis

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...