Wednesday, August 21, 2013

KESI DHIDI YA LEMA (MB) KUHUSU UCHOCHEZI CHUONI YAHAIRISHWA HADI OCTOBA 1 2013 ,DEAD OF STUDENT,OCD NA MAKAMU MKU WA CHUO MASHAHIDI MUHIMU.



 Mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha imeahirisha shauri la kesi inayomkabili Mbunge wa Jimbo la Arusha Mjini, Mh Godbless Lema (CHADEMA), kwa tuhuma za kuchochea vurugu katika Chuo cha Uhasibu Arusha (IAA)  hadi Octoba 1, 2013 ambapo mashahidi wa upande wa mashitaka wataanza kutoa ushahidi wao kwa siku mbili mfululizo.

[DSC09072%255B7%255D.jpg]

mashahidi wa kesi ya uchochezi inayomuhusu mbunge wa jimbo la Arusha  Godbless Lema ,Nyuma ni mshauri wa wanafunzi (Dean of student) akizungumza na Ispekta  Bernad.

Akitoa uamuzi huo mapema leo asubuhi Hakimu Devota Msofe alisema kwamba ameridhia ombi la Wakili wa Mh Lema aliyeomba shauri hilo liahirishwe kutokana na mteja wake kuwa mgonjwa.

 Hakimu Msofe aliwataka mashahidi wote kama walivyohuduria leo kufika Mahakamani hapo siku ya Jumanne na Jumatano ya Oktoba 1 na 2 kwa ajili ya kuanza kutoa ushahidi wao, zoezi ambalo lilipangwa kuanza leo kama kuningekuwa na udhuru wa kuahirisha shauri hilo.
[DSC09071%255B6%255D.jpg]

Mashahidi wa upande wa mashitaka .anaeongea na simu ni Makamu Mkuu wa Chuo cha IAA, Bw Faraj Kasidi na anaemtazama ni Jane Chibuga.

Mashahidi wa upande wa Jamhuri waliofika Mahakamani hapo ni pamoja na OCD wa Wilaya ya Arusha Mjini, Giresi Muroto na Mlezi wa Wananfunzi chuoni hapo Bw John Joseph Nanyaro.

Wengine ni Inspekta wa Polisi Bernad Nyambalya, Makamu Mkuu wa Chuo cha IAA Bw Faraj Kasidi na Jane Chibuga.

Awali Wakili Kimomongoro anayemwakilisha Lema wakisaidiana na Wakili Humrefy Mtui aliwasilisha ombi la kuiomba Mahakama iahirishe shauri hilo hadi tarehe nyingine kwa kile alichoeleza kuwa ni kutokana na Mh Lema kuwa katika hali ya kuumwa na kwamba ni jana tu aliruhusiwa kutoka hospitali ya AICC alikokuwa amelazwa tangia Agosti 14 akiendelea kutumikia siku 10 alizopewa na daktari za mapumziko ya kitandani.
[DSC09076%255B7%255D.jpg]

Inspekta Bernad Nyambalya akisalimiana na Mawakili wa Mh Lema mara baada ya kesi hiyo kuahirishwa. Kulia kabisa ni Mwanasheria Glory Kaaya. Picha zote na Seria Jr.

Wakili Kimomongoro alimkabidhi mwanasheria wa Jamhuri nakala ya “Discharge Summary” kutoka hospitali ya AICC nae akaipitia na kuridhia shauri hilo kuahirishwa kutokana na sababu hiyo ya ugonjwa.

No comments:

Post a Comment

AddThis

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...