Katibu wa bodi ya filamu nchini Bi Joyce FISOO akionyesha bango la filamu mpya "TABIA'' mara baada ya kuzindua filamu hiyo jijini hapa.Baadhi ya wasanii maarufu wakisikiliza hotuba ,wakati wa hafla hiyo .Baadhi ya wasanii na wageni waalikwa wakiangalia filamu hiyo mara baada ya kuzinguliwa na katibu mtendaji wa bodi ya filamu nchini bi JOYCE FISSOO
Uzinduzi
wa filamu hiyo ulifanyika hivi karibuni katika Ukumbi wa Hoteli ya May Fair
Plaza uliopo Mikocheni jijini Dar es Salaam.
Katika
unzinduzi wa filamu hiyo, Bi Fissoo amebainisha kuwa filamu ya TABIA
imekaguliwa na Bodi ya Filamu na kupewa daraja 13 yaani filamu hii inaruhusiwa
kutazamwa na watu kuanzia miaka 13 na kuendelea
“Ni
filamu inayoweza kuonwa na wanajamii wengi kwani imejikita katika kuelimisha
kuanzia kwa watoto wetu”. Alisema Bi. Fissoo.
Bi
Fissoo alisema kuwa hapa nchini ni filamu chache zinazojikita katika kundi hilo
ambazo zinawasilishwa Bodi ukilinganisha na zile zinazolenga umri wa miaka 18
na kuendelea.
Aidha, Bi Joyce ameipongeza Kampuni ya Harmony kwa kuthubutu kwao na ana
imani kuwa Kampuni hiyo itaendelea kuzalisha filamu bora zenye weledi, maadili
na zinazoweza kuingia katika soko la ushindani.
Filamu ya TABIA ni filamu mpya iliyoandaliwa na kutengenezwa na Kampuni
ya Harmony ambayo ni moja ya kampuni iliyowekea kazi zake stamp za TRA ambazo
lengo lake ni kuondokana na wizi wa kazi za wasanii hapa nchini.
|
Wednesday, August 21, 2013
FILAMU MPYA YA “TABIA” YAZINDULIWA JIJINI DAR ES SALAAM
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment