Wednesday, December 12, 2012

WANANCHI WATUNGUANA KWA MAWE KWEYE MKUTANO WA MAONI YA KATIBA MPYA

 Baadhi ya wakazi wa Shehia ya Magogoni wakisubiri kutoa maoni huku wakinyeshewa mvua licha ya kujikinga na viti, yote hiyo ni kuepuka kukosa fursa ya kutoa maoni ya Katiba kwa kuzungumza ana kwa ana na wajumbe wa Katiba. Mvua iliisha wakati muda wao wa kutoa maoni umekwisha hivyo walitumia fomu kuandika na kuwasilisha maoni yao. (Picha: Editha Majura via Mwananchi)

Mkutano wa kukusanya maoni kuhusu mabadiliko ya Katiba mpya ya Muungano umevunjika kwa mara ya pili baada ya kutokea vurugu kubwa katika wilaya ya Mjini, Zanzibar huku mtu mmoja akijeruhiwa kwa kitu chenye ncha kali.

Vurugu hizo zilitokea kwa mara ya kwanza katika uwanja wa Mzalendo, Jimbo Magomeni juzi na Uwanja wa Mpendae mkoa wa Mjini Magharibi Unguja na kujirudia jana.

Jumatatu wiki hii kulizuka mvutano baina ya makundi mawili yenye misimamo tofauti juu ya mfumo wa Muungano; kuna wanaopinga na wanaoukubali. Misimamo hiyo imeelezwa kujikita katika misingi na sera za vyama vyao vya kisiasa

Katika misimamo hiyo, CUF kinaamini katika Serikali ya Zanzibar na Tanganyika kila moja kuwa na mamlaka kamili katika Umoja wa Mataifa na Muungano uwe wa mkataba wakati, CCM kinasimamia kwenye Serikali mbili; Muungano na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.

Mjumbe wa Tume, Ali Saleh, alikiri tume hiyo kushindwa kusikiliza maoni ya wananchi wa Shehia za Jimbo la
Magomeni, kutokana na viongozi wa vyama vya siasa kuingilia shunguli za Tume.

“Ni kweli juzi hapo katika uwanja wa Mzalendo, Tume ilishindwa kupokea maoni ya wananchi baada ya kuibuka vurugu ambazo sisi tunahisi kwamba zinasababishwa na viongozi wa kisiasa,” alisema Saleh, ambaye pia ni mwandishi wa habari mwandamizi nchini.

Akifafanua zaidi alisema kilichojitokeza ni kuwepo kwa mvutano na malumbano kwa viongozi wa vyama vya siasa, ambao wamekuwa wakiifuata Tume kila inapokwenda kupokea na kusikiliza maoni ya wananchi.

Alisema limejitokeza tatizo ambapo baadhi ya wananchi wamekuwa wakitoa maoni katika Shehia ambazo sio zao, ingawa hilo alisema sio tatizo kubwa.

“Tunacholalamika sisi Tume ni viongozi wa vyama vya siasa kuingilia kati na kuratibu kazi ambazo sio zao,” alisema Saleh na kuongeza kwamba kila mwananchi yupo huru kutoa maoni sehemu yoyote mbele ya Tume, hata kama haishi katika eneo lile.


                 

No comments:

Post a Comment

AddThis

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...