Tuesday, December 4, 2012

MWANAFUNZI AFA KWA KUANGUKIWA NA UKUTA WAKATI AKIPITA NJIA ZA PANYA KUONA MTIKISIKO IRINGA


Sehemu ya ukuta uliobomoka

Mwanafunzi wa kidato cha pili katika shule ya sekondari Kwakilosa katika Manispaa ya Iringa Daniel Yona (15) amefariki dunia baada ya kuaungukiwa na ukuta wa uwanja wa Samora wakati akijaribu kupita mlango wa panya ili kwenda kushuhudia tamasha hilo la Mtikisiko 2012.


Tukio hilo lilitokea usiku wa kuamkia Desemba 2 mwaka huu wakati wapenda burudani katika mkoa wa Iringa walipofika katika uwanja huo kushuhudia onyesho kubwa la Mtikisiko 2012 ambalo lilikuwa limepambwa na wasanii mbali mbali wakiongozwa na mkongwe Juma Nature na Profesa J.


Wakielezea kilichomkuta mwanafunzi huyo baada ya mashuhuda walisema kuwa mwanafunzi huyo na wenzake waliacha kupita katika mlango wa kawaida kwa kulipia kiingilio halali kilichowekwa na badala yake aliamua kupita gizani na kupanda ukuta huo wa uwanja wa Samora ili kuweza kuingia ndani ya uwanja huo kuona tamasha la Mtikisiko.

Sehemu ya ukuta iliyobomoko na kusababishaa kifo cha mwanafunzi mmoja

"Ujue hapa vijana wa kihuni kutoka Kitanzini walikuwa wamejipanga hapa na kufanya ufisadi wa kuwatoza watu kiingilio bila wahusika wa Tamasha hilo kujua kinachoendelea .....hivyo hata huyo mwanafunzi alikuwa ni mmoja kati ya wavamizi wa Tamasha hilo kwa kupita njia ya panya ili kuingia ndani ya uwanja huo" alisema mmoja wa mashuda mbaye hakutaka jina lake litajwe

No comments:

Post a Comment

AddThis

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...