Katibu Mkuu wa zamani wa Umoja wa Mataifa, Kofi Annan na Rais Mustaafu wa Tanzania Benjamin Mkapa |
Katibu Mkuu wa zamani wa Umoja wa Mataifa, Kofi Annan na Rais
Mustaafu wa Tanzania Benjamin Mkapa wamekanusha madai kwamba wanaingilia
masuala ya ndani ya Kenya.
Wawili hao wamesema hayo kwenye mkutano wao na waandishi wa
habari mjini Nairobi.
Mkapa na Annan wako
nchini Kenya kwa niaba ya Jopo la Shaksia Mashuhuri kufuatilia mkakati
uliowekwa na serikali ya Kenya kuhakikisha uchaguzi mkuu unafanyika kwa njia ya
uwazi.
Mkapa amesema jukumu lao ni kuona makubaliano ya kitaifa ya
amani ya mwaka 2008 yanatekelezwa ili kuepuka machafuko ya kisiasa baada ya
uchaguzi mkuu ujao.
Kofi Annan kwa upande wake amesema, Kenya ni nchi huru na wao
ni marafiki tu wa nchi hiyo na wala hawana nia ya kuanisha mustakabali wake wa
kisiasa.
Wanasiasa kadhaa wamekuwa wakidai kwamba Annan na wenzake
wamekuwa wakitoa matamshi yanayoonyesha kuwa, wanaingilia mambo ya ndani ya
Kenya.
No comments:
Post a Comment