BAKHRESA ASHIKA NAFASI YA 30 ORODHA YA WATU MATAJIRI BARANI
AFRIKA- FORBES
Bakhresa (kulia) alipokuwa akisalimiana na rais wa Zanzibar Ali Mohamed Shein |
Orodha ya jarida la Forbes la watu 40 matajiri zaidi barani
Afrika imetoa jibu la ‘uhakika’ nani ni mtu tajiri zaidi kuliko wote nchini
Tanzania. Si mwingine zaidi ya Said Salim Bakhresa ambaye amekamata nafasi ya
30 kati ya matajiri 40 wa barani Afrika kwa kuwa na utajiri unaofikia dola
milioni 520 hadi kufikia November, 2012.
Bakhresa ana historia ya pekee kwa kuacha shule akiwa na
miaka 14 na kujiingiza kwenye biashara ndogo ndogo ikiwa pamoja na mgahawa na
biashara ya unga wa kusaga.
Leo hii Bakhresa Group imeajiri zaidi ya watu 2,000 na ni
kampuni kubwa zaidi Tanzania. Bidhaa zake zina umaarufu mno nchini na nje ya
nchi ambazo ni pamoja na unga, vinywaji, ice cream, usafiri wa meli na mafuta
miongoni mwa nyingine.
Kampuni ya Bakhresa ni wazalishaji wakubwa zaidi wa unga wa
ngano Afrika Mashariki na kati ambayo huzalisha kiasi cha 3,200 za tani za
metric. Kampuni yake huendeshwa na wanae wa kiume waliogawana vitengo
mbalimbali.
No comments:
Post a Comment