Karandika lililobeba mahabusu wengine likiwasili mahakamani hapo bila ya mtuhumiwa wa mauwaji ya Daudi Mwangosi |
Mahakama ya hakimu
mkazi wa wilaya ya Iringa imeahirisha kesi hiyo ya mauwaji ya
mwanahabari Daudi Mwangosi ambae pia alikuwa ni mwenyekiti klabu ya
waandishi wa habari mkoa wa Iringa (IPC), mtuhumiwa huyo askari
mwenye namba G2573 Simoni (23) atafikishwa tena mahakamani hapo Desemba 5
mwaka huu kesi hiyo itakapo tajwa tena.
Mwendesha
mashitaka wa jamhuri Adolf Maganda aliieleza
mnahakamani hiyo mbele ya hakimu Dyness Lyimo
kuwa mtuhumiwa huyo mnamo 02 Septemba mwaka huu katika kijiji cha Nyololo
Wilaya ya Mufindi Mkoa wa Iringa alimuua Daudi Mwangosi kwa makusudi kinyume na
kifungu cha sheria namba 148 kifungu kidogo 5A.i cha makosa ya jinai.
Askari polisi wakiweka ulinzi kumziba mwenzao asipigwe picha. |
Taarifa kutoka
mkoa wa Iringa zinaeleza kuwa jeshi la polisi limeendelea kuzuia kutopigwa picha kwa anayetuhumiwa
kuhusika na mauwaji hayo kufuatia kufichwa katika gari maalum na askari
wenzao .
Wanahabari wakiwa wamejipanga kwa picha wakisubiri mtuhumiwa kuletwa mahakamani hapo |
Tukio
hilo lilitokea leo wakati mtuhumiwa huyo akifikishwa mahakamani
huku askari polisi hao muda wote walionekana kuzunguka
huku na kule katika mahakama hiyo kama njia ya kuwathibiti
wanahabari waliokuwepo mahakamani hapo wasipate nafasi ya kumpiga
picha mtuhumiwa huyo
No comments:
Post a Comment