Monday, November 19, 2012

ARUSHA.


WAZIRI MKUU MSTAAFU EDWARD LOWASSA AUNGA MKONO CHADEMA
EDWARD LOWASSA -(MB) CCM WILAYA YA MONDULI


-NI KUHUSU ELIMU BURE HADI SEKONDARI, ASEMA IWE MOJA YA AJENDA ZA CCM 2015

WAZIRI Mkuu wa zamani, Edward Lowassa amesema wakati umefika kwa sasa hapa nchini elimu ya Sekondari iwe elimu bure na kumwondolea mwananchi wa kawaida mzigo wa kubeba gharama za elimu hiyo.

Lowassa akizungumza jana mjini Babati alisema, mjadala kuhusu elimu kutolewa bure hadi sekondari haukwepeki, hivyo kuwataka wadau wa elimu kuanza sasa kujadili suala hilo na kwamba Chama Cha Mapinduzi (CCM) kinapaswa kulifanya hilo kuwa moja ya ajenda zake katika Uchaguzi Mkuu wa 2015.

Alisema elimu ya sekondari ikifanywa bure, itakuwa ni fursa kwa kila mtoto wa Kitanzania kuipata.

 Hatua ambayo itaongeza weledi na uelewa wa mambo mengi katika jamii.

No comments:

Post a Comment

AddThis

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...