RAIS KIKWETE AMLILIA MAREHEMU JACKSON MAKWETA
RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA JAKAYA MRISHO KIKWEWTE AKIWEKA SAINI KITABU CHA MAOMBOLEZO NYUMBANI KWA MAREHEMU JACKSON MAKWETA. |
RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Jakaya Mrisho Kikwete ameshtushwa na kuhuzunishwa na kifo cha aliyekuwa Mbunge mkongwe na Waziri wa miaka mingi katika Serikali za Awamu mbalimbali za uongozi wa Tanzania, Jackson Makweta ambacho kimetokea jioni Jumamosi, Novemba 17, 2012, katika Hospitali ya Taifa Muhimbili, Dar es Salaam.
Katika salamu zake za rambirambi kwa familia ya Mzee Jackson Makwete, Rais Kikwete amemwelezea Mzee huyo kama mtumishi wa umma aliyejali sana ustawi wa jamii yake, mwanasiasa mkweli na mwadilifu, mbunge aliyeleta matumaini kwa aliowawakilisha na waziri aliyetoa mchango mkubwa katika Serikali alizozitumikia.
Rais Kikwete ameiambia familia hiyo ya Mzee Makweta: “Nimepokea kwa mshtuko na huzuni kubwa taarifa ya kifo cha Mzee Jackson Makweta ambacho nimejulishwa kuwa kimetokea jioni ya leo. Kwa hakika Tanzania imempoteza mtumishi wa umma wa mfano na aliyejali sana ustawi wa jamii yake na mwanasiasa mkweli na mwadilifu.”
RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA DOKTA JAKAYA KIKWETE AKIMFARIJI MJANE WA MAREHEMU JACKSON MAKWETA |
Alikuwa kisima cha busara na mzoefu wa uongozi na ameondoka wakati bado tunahitaji sana uongozi na busara zake.”
RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA JAKAYA MRISHO KIKWETE AKITOA HESHIMA ZA MWISHO KUUAGA MWILI WA MAREHEMU JACKSON MAKWETA. |
Namwomba Mwenyeji Mungu, Mwingi wa Rehema, awape subira na uvumilivu ili muweze kuvuka kipindi hiki kigumu. Aidha, naungana nanyi katika kumwomba Mwenyezi Mungu aiweke peponi pema roho ya Marehemu Jackson Makwete. Amina.
No comments:
Post a Comment