Mwezeshaji katika mafunzo ya Ujasiriamali
katika Wiki ya Ujasiriamali Duniani Austin Makani (kushoto) akitambulisha meza
kuu wakati wa Hafla ya kukabidhi vyeti kwa wahitimu na kufunga Mafunzo hayo.
Mgeni rasmi Mkuu wa Shule Kuu ya Biashara ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam Dkt.
Ulingeta Mbamba (katikati), Mratibu Mipango wa Kitengo cha Ujasiriamali cha
Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDEC) Bw. Elia Yobu (kulia), Makamu Mwenyekiti wa
ZAYEE Bw. Omar Said Shabaan (wa pili kulia), Mkurugenzi Mkuu wa Professional
Approach Development Bi. Lillian Secelela Madeje (kushoto) na Katibu Mkuu wa
Shirika Lisilo la Kiserikali la ZAYEE (Zanzibar Association for Youth Education
and Empowerment) Fatma Mabrouk Khamis (wa pili kushoto).
|
Pichani Juu na Chini ni Mkuu wa Shule Kuu ya
Biashara ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam Dkt. Ulingeta Mbamba akitoa hotuba
wakati wa kufunga mafunzo ya Ujasiriamali kwa Vijana yaliyoandaliwa na Asasi ya
ZAYEE (Zanzibar Association for Youth Education and Empowerment) na kutolewa na
Kitengo cha Ujasiriamali cha Chuo Kikuu cha DSM (UDEC).
Dkt. Mbamba amesema mafunzo hayo ni muhimu sana
kwa vijana kwa kuwa yatawawezesha kufanya kazi zao kwa ufanisi, umahiri, tija
zaidi na yatawasaidia sana katika kufanya shughuli zao za kila siku ziwe za
kujiajiri wenyewe au kuajiriwa.
Katika mafunzo hayo jumla ya vijana 103 (68
kutoka Dar es Salaam na 35 kutoka Zanzibar) wamejifunza mambo mengi pamoja na
Ujasiriamali, Fursa za Biashara zilizopo na Changamoto zake, Jinsi ya kupata
Wazo la Biashara pamoja na Mpango wa Biashara.
|
Katibu
Mkuu wa ZAYEE Bi. Fatma Mabrouk Khamis akiwapa nasaha wakufunzi wa mafunzo ya
Ujasiriamali na kuwataka elimu waliyoipata hapo ikazae matunda katika kazi na
biashara wanazozifanya ili kuongeza tija itakayosaidia kukuza uchumi binafsi wa
Taifa.
Pia
ameahidi kuwafikia vijana wa Mikoani kuwapa mafunzo ya Ujasiriamali yatakayowezesha
kuimarisha biashara zao.
Pichani
Juu na Chini ni baadhi ya washiriki wa mafunzo ya Ujasiriamali wakipokea vyeti
baada ya kuhitimu.
Wahitimu wa Global Entreprenuership Week
Tanzania katika picha kumbukumbu pamoja na mgeni rasmi pamoja na wawezeshaji.
|
No comments:
Post a Comment