Mwenyekiti wa Msikiti wa Jamaat Shia Ithna Asheri Bw. Azim Dewji akifafanua kwa waandishi wa habari amesema katika kuadhimisha siku hii Waislam wa dhehebu la Shia watafanya matembezi kutoka makaburi ya Shia Kisutu hadi katika msikiti mkuu wa Shia Ithna Asheri na wakati wa matembezi hayo ndani yake kutakuwa kunafanyika kumbukumbu kwa njia ya kuimba nyimbo za maombolezo tukikumbuka shujaa wetu namna alivyouwawa na vile vile sisi kujipa uhai kiroho katika kuonyesha namna kiongozi anaweza kujitolea kwa watu wake na kwamba ni funzo kwa kila mwanadamu ajitolee kwa ajili ya wenzake. |
Imamu
wa Msikiti wa Imam Ali wa Magomeni Mapipa Msabaha Shaaban Ali Mapinga
akizungumza na waandishi wa habari amesema siku hii ni siku ya
kukumbuka na kuadhimisha miaka 1473 ambapo katika nchi ya Iraq kwenye
mji wa Karbala aliuwawa mjukuu wa Mtume Mohammed (S.A.W) aliyekuwa
akijulikana kwa jina la Imam Hussein Bin Ali Bin Abutwalib.
Amesema katika
nyakati hizo alitokea mtawala dhalim aliyekuwa akitetea dhulma na
kukiuka haki za binadamu kitendo ambacho mjukuu wa Mtume Imam Hussein
hakukubaliana nacho na kuunda jeshi lake dogo kutetea haki na kupinga
Batili.
Kwakuwa Imam Hussein
alikuwa na dhamana ya kutetea haki alikataa kuwa chini ya mtawala huo
ndipo alipotumiwa jeshi la watu kama 30,000 naye akiwa na jeshi la watu
72 walipambana katika mji huo na mjukuu wa Mtume aliuwawa kifo cha
kikatili cha kutenganishwa kichwa na kiwiliwili.
|
Kwa
Upande wake Sheikh Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Alhad Mussa Salum
amesema siku hii ni muhimu sana kwa Waislam kote duniani kwa sababu
tunamkumbuka Imam Hussein ambaye kifo chake kilikuwa ni kifo cha
kinyama, kifo cha wapenda dhulma katika uso wa ardhi.
Amesema kifo cha
Imam Hussein kinamgusa kila Muislam kwa sababu ilikuwa ni siku ambayo
haki ilizimwa na dhuluma, maadui wa haki walijaribu kuitaka batil
isimame , kwa hiyo siku ya leo ni sku ya kutetea haki na uadilifu.
Aidha Sheikh Salum
amesema kwa Waislam wote Tanzania na hata wasio Waislam wanatakiwa
wajifunze kutoka kwa Imam Hussein kwamba yeye alikuwa ni mtetezi wa
haki, alikuwa anatetea Uadilifu kwa hiyo tujifunze kwamba kutetea haki
na kutetea uadilifu ndio jambo linalotakiwa katika maisha ya leo,
kutetea wanyonge, kupiga vita Dhuluma na ukandamizaji wa namna yoyote
ile ndio lililokuwa jambo alilolipenda Imam Hussein.
Pichani juu na chini msafara wa waumini wa Shia umeanza. |
Bango lenye Ujumbe maalum wa siku ya Ashura. |
No comments:
Post a Comment