BAADHI YA RAIA WA MAREKANI WAKIFUATILIA SERA ZA WAGOMBEA URAIS NCHINI HUMO. |
Katika sehemu kubwa ya
mdahalo wao wa muda wa saa moja na nusu ilikuwa juu ya sera ya nje ya
Marekani kuhusiana na Iraq,Afghanistan ,Libya, china Iran na Mashariki ya Kati.
Romney alimlaumu Rais Obama kwa kushindwa kutoa uongozi
unaofaa kwa dunia na kuruhusu amani mashariki ya kati kuvurugika.
Mitt Romney akaanza kwa kumpongeza Rais Obama kwa kumzima Osama Bin Laden
na kwa kuwakabili viongozi wa al-Qaeda, lakini Romney akaelezea kuwa Marekani
haiwezi kuondokana na hatari hiyo kwa njia ya kuua pekee.
Ushindani wa kiuchumi na pamoja na kijeshi baina ya nchi ya
marekani na China ,ni miongoni mwa mambo yaliyodadiliwa huku wagombea wote wakionekana kuunga mkono
ushirika wao na taifa hilo lapili kwa uchumi duniani, lakini Obama yeye
akiongeza kuwa yafaa marekani ikawekeza kwenye elimu pamoja na tafiti ili ili
kuendelea zaidi
Kura za maoni zilizotolewa punde baada ya kukamilika mjadala huo, zilionyesha kuwa rais Obama ni mshindi.
No comments:
Post a Comment